Wananchi wa mtaa wa Mwatulole kituo cha ofisi ya mtendaji wakitafuta majina yao ili waweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Photo: 1/10
Wananchi wa mtaa wa Stop Over Kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo wakiendelea na zoezi la kuhakiki majina kisha kupiga kura. Picha na Sute Kamwelwe
Photo: 2/10
Wakazi wa Kinondoni Mjini wakiangalia majina yao kabla kupiga kura katika kituo cha majengo ya Chuo Biafra, jijini Dar es Salaam. Picha na Sunday George
Photo: 3/10
Photo: 4/10
Photo: 5/10
Mkazi wa kitongoji cha Alaika Kijiji cha Landanai Kata ya Naberera, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Thomas Mamasita akishiriki kupiga kura ya kuwachagua viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji. Picha na Joseph Lyimo
Photo: 6/10
Wananchi kata ya Misheni wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wakiwa wamepanga mstari ili kupiga kura kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa. Picha na Daniel Makaka
Photo: 7/10
Mkazi wa mtaa wa Msangalalee Magharibi Kata ya Dodoma Makulu Jijini Dodoma, Kennedy Chidama akionyesha kidole chake chenye wino baada ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa leo Novemba 27, 2024. Picha na Rachel Chibwete
Photo: 8/10
Wakazi wa kitongoji cha Msikitini mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wakikagua majina yao ili waweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika chini kote leo jumatano Novemba 27 mwaka 2024. Picha na Joseph Lyimo
Photo: 9/10
Baadhi ya wakazi wa kata ya Bweri Manispaa ya Musoma wakiangalia majina yao katika kituo cha kupigia kura cha Bweri FDC kabla ya kuanza kupiga kura. Picha na Beldina Nyakeke