Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kazi za staha ni msingi wa mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

Baadhi ya wawakilishi wa kampuni mbalimbali wakiwa katika warsha ya utatu iliyolenga kuimarisha uhusiano wa kazi kati ya TUICO na waajiri, iliyofanyika Dar es Salaam. Warsha hiyo ilihudhuriwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, na Mahusiano.

Kila mwaka, Siku ya Wafanya­kazi (Mei Mosi) hutoa fursa ya kutambua nafasi ya wafanyakazi, kutafakari viwango vya ajira, na kutathmini mwelekeo wa soko la ajira.

Kaulimbiu ya maadhi­misho ya mwaka huu inasema, “Kazi za Staha ni Nguzo Imara ya Maendeleo Endelevu katika Ute­kelezaji wa Dira ya Taifa 2050.” Kaulimbiu hii inachagiza tafakuri ya kina kuhusu nafasi ya kazi za staha katika uchumi na maende­leo yetu.

Mara nyingi kazi za staha huta­zamwa kama takwa la kijamii, yaani suala linalopaswa kufuati­liwa sambamba na harakati za maendeleo. Hata hivyo, kazi za staha ni kitovu cha uchumi na maendeleo endelevu. Upatikanaji wa ajira zenye tija, haki kazini, ulinzi wa kijamii, na majadiliano ya kijamii ni nguzo kuu za kazi za staha.

Hafla ya utiaji saini Mkataba wa Hali Bora za Kazi kati ya Chama cha Wafanyakazi TUICO na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyofanyika Desemba 19, 2025.

Nguzo hizi zinapokuwa dhaifu, tija na ufanisi hushuka, na ukuaji wa uchumi hukosa usawa, zin­apokuwa imara, uchumi huwa thabiti, jumuishi, na stahimilivu dhidi ya misukosuko.

Nchini Tanzania, nguzo hizi zinadhihirika kupitia Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi­ni, ambayo inaweka msingi wa kisheria wa uhuru wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi, maja­diliano ya pamoja, na viwango vya chini vya mazingira ya kazi. Hata hivyo, ufanisi wa mfumo huu unategemea kiwango cha utekelezaji, ulinzi, na usimamizi wa haki na maslahi ya wafanya­kazi mahali pa kazi.

Kazi za staha ni chachu ya utekelezaji wa dhima ya Dira ya Taifa 2050. Ukuaji wa viwanda, ongezeko la uwekezaji, na kui­marika kwa mtangamano wa masoko ya kikanda na kimataifa vinabadilisha mazingira ya kazi. Wakati huo huo, mahusiano ya ajira yanazidi kugawanyika.

Mkuu wa Sekta ya Viwanda wa TUICO, Innocent Alute (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Cigarette Public Limited Company (TCC Plc), Roy Manalili (kulia), wakibadilishana nyaraka za Mkataba wa Hali Bora

Kampuni zinapeana kandarasi za biashara, ikiwa ni pamoja na kampuni X kukasimu majukumu fulani kwa kampuni Y (outsourc­ing). Ajira zisizo rasmi zinazidi kuongezeka. Hali hii inabadili­sha mifumo ya zamani ya kazi. Ingawa mwelekeo huu unaonge­za unyumbulifu na ufanisi, pia unadhoofisha usalama wa ajira na kupunguza nguvu ya majad­iliano ya pamoja.

Licha ya mazingira ya kazi yanayobadilika, viwango vya kazi vinavyotambuliwa kimatai­fa vinaendelea kuwa muhimu. Kanuni za msingi, kama zilivyoainishwa katika Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) Na. 87 na Na. 98, zinatoa msin­gi wa taasisi unaowawezesha wafanyakazi kujiunga na kushiri­ki katika majadiliano ya pamoja.

Hizi ni nyenzo muhimu zinazow­awezesha wafanyakazi kuathiri vigezo na masharti ya ajira zao na kuchangia mahusiano ya kazi yenye tija, uwiano, na uthabiti.

Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kinaendelea kutekele­za majukumu yake ndani ya muktadha huu. Kazi za Chama hazikinzani na dhima ya Dira ya Taifa 2050; bali ni sehemu ya mifumo inayohakikisha maende­leo ya Taifa yanakuwa jumuishi na endelevu. Kupitia uhama­sishaji, uwakilishi, na majadilia­no ya pamoja, TUICO inachan­gia kuboresha mazingira ya kazi katika sekta mbalimbali za uchu­mi.

Katibu Msaidizi wa TUICO, Hassan Mtyota akitekeleza majukumu ya uhamasishaji kwa wafanyakazi katika kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Company Limited, kilichopo jijini Dar es Salaam.

Jitihada za TUICO zimejikita katika kupanua uwakilishi na kuimarisha ushiriki wa wana­chama mahali pa kazi. Hali hii inaonekana katika ongezeko la wanachama, ambapo idadi imefikia zaidi ya 140,000 nchi nzima kufikia Desemba 2025, ikilinganishwa na 132,794 mwezi Januari. Ongezeko hili, pamoja na ziara na uhamasishaji kazini, linaendelea kupanua uwakilishi katika sekta mbalimbali, ikiwe­mo zile zisizo na mifumo rasmi.

Majadiliano ya pamoja yanaendelea kuwa chombo kikuu katika mchakato huu. Mikataba 59 ya hali bora za kazi iliyosain­iwa katika miezi sita iliyopita imeboresha mishahara na hali za kazi, huku ikiimarisha utabirika na uthabiti katika mahusiano ya kazi.

Wakati huo huo, mabaraza ya wafanyakazi na mifumo ya utatuzi wa migogoro imeweze­sha kushughulikia migogoro na malalamiko 331 ya kazini kwa njia ya usuluhishi. Kesi nyingi zimetatuliwa kupitia majadilia­no ya ana kwa ana bila kufikish­wa katika hatua za juu zaidi.

Vilevile, kujenga uwezo wa wanachama na watendaji ni kipaumbele. TUICO imewekeza katika programu za mafunzo na semina ili kuwajengea wanacha­ma, wafanyakazi, na wawakilishi wao uelewa na ujuzi wa kushiriki kikamilifu katika majadiliano na kutekeleza haki zao. Katika miezi sita iliyopita, semina 1,200 zime­fanyika, zikichangia kuimarisha ubora wa uwakilishi na ushiriki katika michakato ya kiuchumi.

Jitihada hizi zinafanyika kati­ka soko la ajira linaloendelea kubadilika. Kuongezeka kwa aji­ra zisizo za kimikataba, kukua kwa sekta isiyo rasmi, na ushaw­ishi wa mitandao ya uzalishaji ya kimataifa vinahitaji mbinu mpya za uhamasishaji.

Hii ni pamoja na kupanua wigo wa uhamasishaji katika sekta mpya na ambazo hazijafikiwa ipasavyo, kuimarisha majadilia­no ya pamoja yanayotegemea taarifa, na kuimarisha majadilia­no ya kijamii.

Sambamba na hilo, TUICO inaendelea kuimarisha mifumo ya kitaasisi, ikiwemo matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), ili kuboresha ufanisi na usahihi wa taarifa na kuhakikisha hatua zin­azochukuliwa zinaendana na hali halisi ya soko la ajira.

Wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO na Menejimenti ya Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kikao shirikishi kilichofanyika Januari 19, 2026 katika katika Hotel ya Parrot jijini Arusha.

Juhudi za pamoja zinahitajika. Serikali inapaswa kuhakikisha utekelezaji thabiti wa mfumo wa kisheria. Waajiri wanapas­wa kuoanisha shughuli zao na viwango vya ajira vinavyozin­gatia haki na uendelevu mahali pa kazi. Wafanyakazi wanapas­wa kuendelea kuimarisha mshi­kamano na kushiriki kikamilifu katika kudai, kulinda, na kutetea haki na maslahi yao.

Kwa ujumla, kazi za staha ni miongoni mwa masharti ya msingi ya ujenzi wa uchumi na maendeleo jumuishi, shindani, na endelevu—mwelekeo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.