Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kusukuma mbele kauli ya ‘Kilimo ni Biashara’ kupitia Ajenda 10/30: Mafanikio ya Wizara ya Kilimo kupitia COPRA

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza bungeni alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/ 2026, jijini Dodoma Mei 22, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi


Wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo ya Sh1.243 trillioni Mei 20, Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe alisema ili kusimamia vyema maendeleo ya uzalishaji na mnyororo wa thamani wa nafaka na mazao mchanganyiko, Serikali ilirekebisha Sheria ya Usalama wa Chakula ya mwaka 1991 kupitia Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ya mwaka 2009.

Marekebisho hayo yalianzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA). Alibainisha kuwa Serikali ilichukua hatua hii mahsusi kufuatia mabadiliko ya Sera ya Kilimo kuelekea “Kilimo Biashara” na dhamira ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula duniani.

COPRA pia inasimamia mazao yote ambayo hapo awali yalitambulika kama mazao ya chakula kwa kuhakikisha kunakuwa na mifumo imara inayosimamia ubora unaohitajika na masoko ya uhakika kote duniani. Juhudi hizi zinachangia ongezeko la tija na ukuwaji wa sekta ya kilimo.

Ili kusisitiza wajibu wa Serikali katika kuhakikisha usalama wa chakula na kutumia kikamilifu nafasi ya Tanzania katika ushindani barani Afrika, ilikuwa muhimu kuanzisha COPRA ili kuunda mifumo ya kisheria ya ufunguaji wa masoko kwa kuweka mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji kwa ajili ya ukuaji wa sekta ya kilimo.

Mbali na mazao ya biashara ya asili kama chai, sukari, kahawa, pamba, mkonge, tumbaku na korosho COPRA inasimamia mazao mengine yote yanayolimwa Tanzania hususani nafaka na mazao mchanganyiko.

Mazao hayo ni pamoja na nafaka zenyewe, matunda, mbogamboga, mazao ya bustani, viungo na vikolezo, mbegu za mafuta kama ufuta, karanga, alizeti na chikichi, mazao ya mizizi kama mihogo, magimbi, viazi mviringo, viazi vitamu, pamoja na mikunde kama maharage, kunde, choroko, mbaazi, dengu na soya.

Hii inajumuisha majukumu ya kuwatambua na kuwarasimisha wadau wote walio kwenye mnyororo wa thamani kwa kufanya usajili na utoaji wa leseni kwa wakulima, wafanyabiashara, maeneo ya biashara ya pamoja, utoaji wa miongozo inayosimamia biashara na kutoa vibali vya uingizaji na usafirishaji wa mazao yaliyo chini ya mamlaka yake.

“Tangu kuanzishwa kwake, COPRA imetoa vibali vya kusafirisha nje tani milioni 3.7 za mazao. Hizi zinajumuisha vibali 1,189 kwa tani milioni 3 za mahindi, vibali 929 kwa tani 564,592 za mpunga, na vibali 540 kwa tani 112,882 za maharage,” alisema Mhe Bashe.

Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi Irene Mlola.

Mhe Bashe aliongeza kuwa Wizara ipo kwenye hatua ya kukamilisha kanuni nne za usimamizi wa nafaka na mazao mchanganyiko ambazo ni: Kanuni ya udhibiti wa ubora; Kanuni ya usajili, leseni na utoaji wa vibali; Kanuni ya kilimo cha mkataba na kanuni mahsusi ya usimamizi wa zao la parachichi. Alisema kanuni hizi zinatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.

Aidha, alisema COPRA imeanza kutekeleza mpango wa elimu kwa umma katika mikoa yote ya Tanzania na kuelimisha juu ya miongozo mbalimbali ya kusimamia biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko.


Malengo kabambe kwa 2025/2026

Kwa msimu wa 2025/2026, Wizara inapanga kuongeza uzalishaji wa zao la ufuta kutoka tani 200,000 hadi tani 250,000, na zao la kakao kutoka tani 13,652 hadi 15,000. Pia, juhudi za kimkakati zitaimarisha biashara ya mbaazi, ufuta, na parachichi mazao yaliyopata mapato ya dola za Marekani bilioni 3.54 katika mwaka wa 2023/2024 pamoja na kahawa, pamba, tumbaku na korosho. Kati ya haya, mazao matatu yako chini ya usimamizi wa COPRA, huku mengine yakisimamiwa na bodi husika.

Miongoni mwa mafanikio haya, uzalishaji wa parachichi umeongezeka kufikia tani 195,162 wakati mauzo yake nje ya nchi yakiongezeka kutoka tani 26,826 mwaka 2022/2023 hadi tani 35,627 mwaka 2023/2024, asilimia 118.7 ya lengo la tani 30,000.

Waziri Bashe alisema COPRA itasajili wakulima 91,000 wa kakao katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Tanga, na kugawa miche milioni moja ya kakao kwa mfumo wa ruzuku.

Katika mwaka 2023/2024, Wizara ikishirikiana na COPRA pamoja na wadau imesaidia uzalishaji wa tani milioni 7.5 za mazao ya bustani sawa na asilimia 83.5 ya lengo la tani milioni tisa. Mafanikio haya yametokana kusimamia mifumo mizuri ya biashara na ufunguaji wa masoko ya kimataifa pamoja na mafunzo kwa maafisa ugani na wakulima.

Mafanikio haya yametokana na kusimamia vizuri mifumo ya biashara na ufunguaji wa masoko ya kimataifa pamoja na mafunzo kwa maafisa ugani 250 na wakulima 1,200.

Katika msimu ujao, Wizara ya Kilimo itaendelea kutekeleza mkakati wa kukuza sekta ya mazao ya bustani, ikilenga kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani milioni 9.

Ili kufanikisha lengo hili, juhudi zitaelekezwa katika kusimamia ubora wa mazao na kuimarisha mifumo ya masoko.

Kwa upande wa zao la parachichi, jumla ya miche milioni 2.1 inatarajiwa kuzalishwa na kusambazwa kwa wakulima kupitia mpango wa ruzuku.

Vilevile, ujenzi wa maghala ya kuchakata mazao (packhouses) matatu pamoja na vituo 100 vya ukusanyaji mazao (collection centers) unatarajiwa kukamilika ili kuimarisha mnyororo wa thamani.

Aidha, mafunzo mahsusi yataandaliwa kwa maafisa ugani wanaohudumia zao la parachichi, sambamba na kuanzishwa kwa mfumo wa BBT-Ugani katika maeneo ya uzalishaji.

Lengo ni kuhakikisha wakulima wanapatiwa huduma za kitaalamu na kusimamiwa ipasavyo ili kufanikisha uzal­ishaji wenye viwango bora unaokidhi soko la ndani na la kimataifa.

Ili kukabiliana na visumbufu vya parachi­chi, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) itanunua na kusambaza lita 3,000 za viuatilifu na lita 1,000 za copper sulphate kupitia mpango wa ruzuku.

Maoni ya Wabunge

Akichangia, Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Agnes Hokororo (CCM), alisifu jitihada za serikali kuboresha upatikanaji wa pem­bejeo na huduma za ugani, lakini akaomba zirejeshwe wizarani na kuanza mchakato wa kuanzisha Wakala wa Ugani.

Alisema msimu uliopita korosho ziliuzwa kwa wastani wa Sh3,500 hadi Sh4,195 kwa kilo katika soko la TMX, huku mbaazi zikiuzwa kati ya Sh1,800 na Sh2,200 kwa kilo.

“Nataka kumwambia Mheshimiwa Bashe kuwa kazi aliyoifanya Mheshimiwa Rais, Dk Samia Suluhu Hassan mkoani Mtwara hai­japata kutokea. Sisi tunaishukuru serikali anayoiongoza,” alisema.

Mhe. Sophia Mwakagenda (CHADEMA) ali­sifu mafanikio ya kilimo cha parachichi Run­gwe na kupongeza uongozi wa Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi Irene Mlola.

“Mheshimiwa Waziri uliwaleta ndugu zetu wa COPRA na dada Irene (Madeje Mlola-Mku­rugenzi Mkuu) amekuwa mwaminifu. Ame­fanyakazi kwa nguvu sana kuhakikisha yale machungu ya kuuza parachichi kwenye viroba yanakoma. Naamini msimu ujao watasimamia vizuri zaidi,” alisema.

Mbunge wa Nsimbo, Mhe. Anna Lupem­be (CCM) alihimiza utoaji wa elimu kwa wakulima wa ufuta Katavi kabla ya kuingizwa kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani.

“Niishukuru Serikali kwa kazi kubwa ambayo inaendelea kufanywa. Tunaona kwenye mikoa mingine kama Mtwara, Lindi, wananchi wanapata manufaa makubwa kupi­tia mfumo wa stakabadhi ghalani,” alisema.

“Mmeomba mkoa wa Katavi tuingie kwenye stakabadhi ghalani mwaka huu, na wananchi bado hawajazoea, hili jambo ni geni kwao. Naomba sana Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye elimu,” alishauri.

Mhe. Lupembe alibainisha kuwa wanan­chi wamezoea kuuza kiholela, na kwamba uhamasishaji wa waheshimiwa wabunge umewapa hamu nao kunufaika.

“Licha ya kulima sana ufuta msimu huu, mfumo huu umewakuta wananchi wakiwa wamezoea mfumo wa kizamani. Ombi letu ni kuwa elimu itolewe kwanza,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Mwand­abila, (CCM) aliipongeza Serikali kwa mpan­go wake wa kuzalisha na kugawa miche ya parachichi kwa wakulima katika msimu wa 2025/26 pamoja na kujenga viwanda vya kuchakata bidhaa zisizofaa kuuzwa nje ya nchi.

“Kwetu tuna mwekezaji aitwaye Lima. Anatusaidia kupunguza burden (mzigo) wa parachichi ambazo hazijafikia viwango vya ubora wa kuuza nje ya nchi,” alisema.

“Kupitia forum (jukwaa) hili napenda kukuomba Mheshimiwa Bashe na timu yako tazameni namna ya kuisaidia Lima kutumia vizuri fursa hii kwa sababu licha ya mafuta, tunaweza kuzalisha bidhaa nyingine nyingi ikiwemo mbolea,” aliongeza.


Wajibu wa COPRA na maono ya taasisi

Katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi Irene Mlola, alisema taasisi yake inalen­ga kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kurasimisha biashara ya mazao yasiyo na bodi maalumu.

“Kwa muda mrefu, Watanzania wamechukulia mazao ya chakula kama siyo biashara. Lakini chini ya Rais Mhe Dk Samia, uwekezaji mkubwa umefanyika kuhakikisha mazao haya yanaleta faida,” alisema.

“COPRA inahakikisha masoko yenye mfumo thabiti na viwango bora, ikiendana na Ajenda 10/30 na falsafa ya ‘Kilimo ni Biashara’ kuhaki­kisha Tanzania inakuwa na ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa,” aliongeza.