Kutoka Cameroon hadi Urusi: Safari ya Essaga ya kutafuta mafanikio na kuungana tena na mama yake
Mara kwa mara tumekuwa kusikia simulizi za washiriki wa mpango wa Alabuga Start. Wasichana kutoka Afrika, Asia, na Amerika ya Kusini wanazungumzia kuhusu kazi, kuzoea maisha nchini Urusi, changamoto ya lugha, hali ya hewa na pia jinsi wanavyozikumbuka familia zao. Kwa kawaida, washiriki hao husafiri kwa ndege kurudi kwao wakati wa likizo. Lakini safari hii, mama wa mmoja wa washiriki alikuja kumtembelea mwanawe.
Atouma Marie alisafiri kwa ndege hadi Urusi, ambako ukanda maalum wa kiuchumi wa Alabuga unapatikana. Binti yake, Essaga mwenye umri wa miaka 21, amekuwa akifanya kazi katika programu hiyo kwa mwaka mmoja sasa. Mama wa mshiriki huyo alizungumza kuhusu hisia za mzazi anapomruhusu mtoto wake kwenda mbali zaidi na nyumbani kufanya kazi. Na nini hutokea wakati mama anapoona namna binti yake anavyoishi katika eneo hilo.
“Kwa nini isiwezekane?” – jinsi mama alivyokubali kumruhusu binti yake aende Urusi
Atouma Marie ni mjasiriamali kutoka Cameroon na mtu mwenye mtazamo wa wazi kuhusu ulimwengu. Urusi haikuwa nchi ngeni kabisa kwake: aliwahi kufika huko hapo awali na amejionea jinsi vijana wanavyofanya kazi. Wakati binti yake mkubwa Essaga alipopata fursa ya kwenda Urusi kupitia programu ya Alabuga Start, alimuunga mkono.
“Niliwaza, vyema, kwa nini isiwezekane? Hii ni fursa kwake kupata uzoefu, kujitegemea, kujifunza lugha na kujijengea mustakabali wake”, anasema Atouma Marie
Bila shaka, kama mzazi yeyote, alikuwa na wasiwasi. Safari ya kwanza ya mbali, nchi tofauti, hali ya hewa mpya na lugha ngeni vilisababisha hofu. Lakini nia ya kumpa binti yake nafasi ya maisha mapya na maendeleo ilikuwa na nguvu zaidi kuliko hofu yake. Essaga mwenyewe anakiri kwamba siku za mwanzoni nchini Urusi ilikuwa wakati wa mabadiliko makubwa kwake.
“Mwanzoni ilikuwa vigumu sana kwangu. Sikumjua mtu yeyote, kulikuwa na kikwazo cha lugha, kila kitu kilikuwa kipya karibu nami,” anaeleza msichana huyo.
Kipindi cha majira ya baridi kilikuwa cha kushangaza zaidi. Baada ya kutoka kwenye mazigira ya joto kali nchini kwao Cameroon, theluji na baridi vilikua changamoto nyingine kwenye maisha yake nchini Urusi. Lakini polepole, maisha yalianza kubadilika: Essaga alikutana na wasichana kutoka nchi tofauti, akapata marafiki na kuanza kujiamini zaidi.
Kuna tamaduni nyingi tofauti hapa. Shukrani kwa hili, nilikutana na wasichana kutoka sehemu mbalimbali duniani. Tunasaidiana, tunatoka pamoja, tunazungumza tunashirikishana, anasema mshiriki huyo wa programu ya Alabuga Start.
Ilikuwa nchini Urusi ambapo Essaga alianza kutumia lugha Kiingereza na Kirusi kwa ufasaha. Programu hiyo ikawa kwake siyo tu uzoefu wa kikazi bali pia kubadilishana utamaduni. Hapa alikutana na wasichana kutoka Brazil, Guinea-Bissau na nchi nyingine ambazo awali hakujua chochote kuhusu nchi hizo.
Chumba kwangu wote walizungumza Kiingereza na Kirusi. Ilinibidi nijifunze kuwasiliana na ilinisaidia sana kukua.
Kukutana tena baada ya mwaka mmoja wa kuwa mbali
Moja ya mambo yaliyogusa hisia zaidi katika mazungumzo na familia hiyo ni pale mama anapokumbuka mshahara wa kwanza wa binti yake.
“Nilifurahi aliponitumia pesa kwa mara ya kwanza. Nilikuwa nimeishiwa kidogo. Kwa hiyo, iliniwezesha kuwapeleka wadogo zake shuleni,” anasema Atouma Marie.
Nchini Cameroon, kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika, ada za shule ni changamoto kubwa kwa familia nyingi. Essaga, akifanya kazi kama mfanyakazi wa usafi nchini Urusi, aliweza kugharamia gharama hiyo. Sasa haikuwa tena wazazi wake wakimsaidia, bali yeye akiwasaidia wao.
Aidha kukutana kwa mama na mototo baada ya kipindi kirefu ilikuwa tukio linguine lililogusa hisia zaidi.
“Najisikia furaha sana. Unapomwona mtoto wako tena baada ya muda mrefu kiasi hicho, unahisi hali ya utulivu na furaha, – anasema Bi Atouma. – Niliweza kuona kila kitu kwa macho yangu mwenyewe. Najisikia kujiamini zaidi sasa. Najua yuko salama.
Ziara ya mama yake ikawa chanzo cha nguvu mpya na motisha kwa Essaga.
“Nilipomwona mama, sikuamini macho yangu. Niliambiwa kwamba angekaa siku moja tu. Kuja kwake kuliamsha mengi ndani yangu: nilipata ujasiri zaidi ndani yangu na nilielewa kuwa naendelea kukua na kujifunza kutokana na maisha,” anasema binti huyo.
Kutoka nje ya eneo ulilozoea kunavyokamilisha ndoto
Hadithi hii si kuhusu siasa au kelele za vyombo vya habari, bali ni kuhusu mambo machache rahisi ambayo mara nyingi tunayasahau. Familia si neno tu; ni mfumo wako wa msaada, ulimwengu mzima unaoweza kukulinda hata katika nyakati ngumu zaidi.
Leo, Essaga anatoka nje ya eneo alilozoea kwa ajili ya familia yake. Anakua kama mtaalamu ili kufikia mengi zaidi na kuisaidia familia yake.
Msichana huyo hakujua Kiingereza wala Kirusi, hakuwa na wazo theluji ni nini na alikuwa hajawahi kufanya kazi katika kampuni ya kimataifa. Leo anazungumza lugha kadhaa, ni rafiki wa wasichana kutoka nchi kumi na anatuma pesa nyumbani.
“Naendelea kujifunza kuzungumza lugha tofauti kwa sababu ni muhimu sana kazini, hata nje ya kazi. Natumaini nitaweza kuongeza mkataba wangu ili niweze kuwa msimamizi (administrator), – msichana huyo anaeleza malengo yake. Kwa sababu ninapowaona wale wanaofanya kazi katika utawala, nimekuwa nikivutiwa sana. Ni kweli kwamba inahitaji juhudi kubwa, lakini mimi pia ningependa kuifanya,”
Mama yake anaunga mkono jitihada za binti yake. Zaidi ya yote, anataka Essaga awe anajitegemea, anajiamini na mwenye furaha. Na kwa ajili hiyo, alikubali kumruhusu aende maelfu ya kilomita, kuvumilia kuwa mbali, ugonjwa wa binti yake mdogo na kisha kupanda ndege na kuona kila kitu kwa macho yake mwenyewe.
Mwishoni mwa mazungumzo, tulimwomba Essaga awaeleze wale ambao wanafikiria tu kutuma maombi.
Wasichana, njooni tu, mtajionea wenyewe, ni program nzuri. Mtakutana na watu wengi wapya. Mtagundua utamaduni wa Kirusi ambao tayari. Urusi ni nchi isiyo ya kawaida, anaeleza mshiriki huyo wa Alabuga Start