Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SimBanking: Daraja la mapinduzi ya huduma za benki kidijitali na uboreshaji maisha ya Watanzania

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (wa pili kulia) akimkabidhi Fahad Soud Hilal wa jijini Tanga, ufunguo na namba ya usajili gari aina ya IST baada ya kuibuka mshindi wa pili katika kampeni ya "Benki ni SimBanking." Wengine katika picha ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd (kulia), Meneja Biashara wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Elikira Nkya (kushoto), mtoto wa Hilal pamoja na Meneja wa Benki ya  CRDB tawi la Dar Village, Isaya Lyimo (wa pili kushoto).

Ni fahari kubwa pale ubunifu wa kibiashara unapokuwa nguvu ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu. Hii ndiyo hadithi ya SimBanking, huduma ya fedha kupitia simu ya mkononi kutoka Benki ya CRDB, ambayo imekuwa mhimili wa ujumuishaji wananchi katika huduma za fedha nchini.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2009, SimBanking imevuka matarajio yaliyokuwapo awali kwa kuwa daraja la kuwaunganisha Watanzania na huduma za fedha ikichochea maendeleo na kuboresha maisha ya kila siku.

Kupitia simu zao za mkononi, wananchi sasa wanaweza kutuma fedha kwenda kwa wapendwa wao, kulipa ada ya shule, kupokea mshahara, kuomba mkopo, na kufanya malipo dukani au sehemu nyingine yoyote inayotoa huduma, bila kulazimika kutembelea tawi la benki.

Mshindi wa tatu wa gari aina ya IST, Salum Juma Mdulu kutoka mkoani Tabora akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa zawadi aliyojishindia. Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (wa kwanza kushoto), Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kulia) na Meneja Biashara wa Kanda ya Magharibi wa Benki ya CRDB, Anselm Mwenda (kulia).

Kupitia SimBanking ambayo inawawezesha Watanzania wasio na akaunti au kadi za benki kufanya miamala kuanzia tawini, kwenye mashine ya kutolea fedha, vituo vya malipo au kwa CRDB Bank Wakala kwa urahisi, mteja anaweza kujua viwango vya kubadilisha fedha za kigeni, kuwekeza kwenye mifuko rasmi ya uwekezaji au kununua hisa za kampuni zilizosajiliwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), hali inayorahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika kuzipambania fursa za kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (wa tatu kulia) akimkabidhi Fahad Soud Hilal wa jijini Tanga mfano wa kadi ya bima kubwa ya gari baada ya kuibuka mshindi wa pili wa gari aina ya IST katika kampeni ya Benki ni SimBanking. Wengine katika picha ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd (wa tatu kushoto), Meneja Biashara wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Elikira Nkya (kushoto), Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Dar Village, Isaya Lyimo (kulia) na Meneja Bima wa CRDB Insurance Company, Omari Melele (wa pili kulia).

Katika kugusa maisha ya watu ambao ni matokeo ya ubunifu wa huduma ya SimBanking, Said Mbaruku Mohamed, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam alikuwa mshindi wa kwanza wa gari mwaka huu.

Baadaye alifuata Fahad Soond Hilal, mfanyabishara wa usafirishaji kutoka jijini Tanga kisha Salum Juma Mdulu kutoka Tabora akawa wa tatu katika orodha ya washindi wanne wa gari aina ya Toyota IST hivyo kubakiza IST moja na Toyota Harrier moja itakayotolewa kwa mshindi wa jumla wa kampeni ya Simbanking mwaka huu.

Zawadi hizi kubwa mwaka huu ni muendelezo wa kile kilichofanywa mwaka jana na misimu mingine iliyopita ambapo wateja wa Benki ya CRDB waliofanya miamala mingi zaidi kupitia Simbanking waliibuka washindi katika vipengele tofauti.

Kwa mwaka 2024 washindi wanne walijishindia magari aina ya Nissan Dualis, sita wakaondoka na bajaj huku 12 wakijipatia pikipiki. Vilevile, washindi 100 walipata simu za kisasa na wanafunzi 10 wa vyuo vikuu walipata kompyuta mpakato.

Alipotangazwa kuwa mshindi wa gari katika droo ya kwanza ya kampeni ya Simbanking ikiwa imekatiwa bima kubwa na kujazwa mafuta ‘full tank,’ Mohamed alisema haamini kama miamala ya kawaida aliyokuwa akiifanya kila siku itakuja kubadilisha maisha yake.

Namshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya kushinda lakini najishukuru mwenyewe kwa kujaribu bahati yangu na hatimaye imekuwa kweli,” anasema.

Mohamed kwa furaha. Siku aliyopigiwa simu na kutaarifiwa kuwa amejishindia gari, Mohamed alikuwa amenunua umeme kupitia Simbanking na anaamini muamala huo uliongeza nafasi yake ya kuibuka mshindi.

Kama walivyo maelfu ya wafanyabiashara wengine wenye nidhamu ya fedha, ni utaratibu wa kawaida kwa Mohamed kuweka fedha za mauzo ya kila siku kwenye akaunti yake ya Benki ya CRDB na anapotaka kuzitumia basi hufanya hivyo kupitia huduma za Simbanking.


Maboresho ya huduma kwa SimBanking

Katika zama za teknolojia, SimBanking ni harakati ya kuleta mageuzi ya kweli ya huduma za fedha nchini kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa vikwazo vya kijiografia, kupunguza gharama, na kuokoa muda wa mteja kukamilisha muamala huku ikifikisha huduma kwa wananchi wote.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul anasema jukwaa hili limeendelea kuboreshwa kwa kuhakikisha huduma zake zinapatikana kwa urahisi, usalama, na kwa haraka zaidi wakati wote na mahali popote alipo mteja, iwe mjini au kijijini hata nje ya nchi.

Kwa sasa, anasema wateja wanaweza kufanya miamala ya hadi shilingi milioni 50 kwa siku, kiwango kilichoboreshwa kutoka shilingi milioni 30 za awali. Pia kuna nafasi ya kuomba kuongeza au kupunguza ukomo wa miamala kati ya shilingi milioni 10 hadi shilingi milioni 20 kulingana na mahitaji ya mteja.

“Ukitaka kutuma, sasa hivi ‘application’ yetu inakuruhusu kuweka mpaka majina ya wapokeaji watano. Hii inawafaa sana wale wanaotuma hela kwa watu wengi, wanaweza kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda mfupi tena kwa gharama nafuu,” anabainisha Bonaventure.

Salum Juma Mdulu kutoka mkoani Tabora akionyesha ufunguo na namba ya usajili wa gari lake aina ya IST baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (katikati). Anayeshuhudia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kulia).

SimBanking sio tu bidhaa ya benki bali ni daraja la fursa linaloleta usawa na matumaini kwa maelfu ya Watanzania wanaotumia huduma zake.

Kwa kuunganisha teknolojia na maisha halisi ya watu, jukwaa hili linaendelea kuwa injini ya mapinduzi ya kijamii na kiuchumi kwa kila mtumiaji wake nchini likimpa fursa za kununua bidhaa kutoka mahali popote duniani sambamba na kumwonyesha viwango vya kubadilishia fedha za kigeni kiganjani mwake.

“Kupitia Simbanking, mteja anaweza kupanga bajeti ya siku, wiki au mwezi hata mwaka mzima. Benki ya CRDB imekuwa ikitoa elimu ya fedha kupitia majukwaa tofauti lakini sasa imeweka sehemu ya mteja wetu kutekeleza elimu aliyoipata kwa vitendo. Kupitia Simbanking unaweza kuweka taarifa za mapato na matumizi yako. Hii inapatikana Benki ya CRDB pekee,” amesema Bonaventura.

Dhamira ya Benki ya CRDB ni kuhakikisha kila Mtanzania anaweza kutumia huduma za benki pasipo kikwazo chochote hususan kipindi hiki ambacho dunia inashuhudia kizazi kinachokua kikiwa tayari hakijawahi kwenda tawi la benki kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani mteja anaweza kufungua akaunti kwa kutumia programu ya Simbanking na akaweka fedha ama kwa wakala au akahamisha kutoka mtandao wake wa simu ya mkononi kwenda benki na kinyume chake.

Mshindi wa tatu wa gari aina ya IST, Salum Juma Mdulu kutoka mkoani Tabora akiwa ameegemea gari lake baada ya kuliegesha nyumbani kwake muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo. Mdulu ameshinda zawadi hiyo baada ya kufanya miamala mingi kupitia SimBanking.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa anasema hata kwa wajasiriamali wachanga wanaolelewa na taasisi hiyo wanayo fursa ya kutumia huduma mbalimbali kupitia Simbanking.

Kwa sasa mteja anaweza kufungua Akaunti ya Imbeju, akahamisha fedha au kufanya malipo na hata kupata taarifa za akaunti yake kupitia Simbanking hivyo hata kama mteja yupo kijijini bado ataendelea kufurahia huduma za Benki ya CRDB bila wasiwasi wowote,” anasema TullyEsther.