Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefuta matokeo ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili za rushwa.

Mbali na Simiyu, lakini CCM kimesimamisha uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kwa mikoa ya Arusha na Mbeya ambao wanatuhumiwa kutembeza rushwa huku wakionya uamuzi wa kufuta unaweza kuendelea katika maeneo yatakayobainika kukiuka sheria.