Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), Habibu Suluo amesema hadi sasa wameshatoa vibali vya muda kwa zaidi ya mabasi 130 ili kutatua changamoto ya usafiri katika kipindi cha sikukuu.

Suluo amesema leo Jumamosi Desemba 24, 2022 baada ya kufanya ukaguzi katika kitua cha mabasi cha Magufuli Mbezi jijini Dar es Salaam.