Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampeni ya Mama Samia Legal Aid awamu ya pili kuzindiliwa Zanzibar

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali  Suleiman akizungumza kuhusu uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Mama Samia inayotarajiwa kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Juni 20, 2026 Dole Mkoa wa Kaskazini Unguja

Muktasari:

  • Baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ikitajwa kuleta mafanikio kwenye jamii, sasa inatarajiwa Juni 20, 2026 kuzinduliwa kampeni nyingine kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Unguja. Baada ya kukamilika awamu ya kwanza ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aids (MSLAC) kwa mafanikio, sasa inatarajiwa kuzinduliwa awamu ya pili ya kampeni hiyo ambapo safari hii itazinduliwa Dole Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kampeni hiyo kwa mara ya kwanza ilitekelezwa kuanzia Aprili 2023 hadi Juni 2025 katika mikoa yote 31 ya Tanzania ambapo kwa kipindi cha mwak wa fedha 2024/25 iliongezewa bajeti kutoka Sh2 bilioni hadi Sh6 bilioni lengo kuwafikia wananchi wengi zaidi ambapo kwa kwa upande wa Zanzibar pekee zaidi ya wanachi 422,908 walinufaika na kampeni hiyo.

Akizungumza kuhusu uzinduzi wa kapmeni hiyo Juni 12, 2026 inayotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Juni 20, 2026, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora, Haroun Suleiman amesema kupitia kampeni hiyo imewasaidia wanachi wanyonge ambao walikuwa hawajui wapi waende na kusaidiwa.

“Kampeni hii ina lna lengo la kuendela kusogeza huduma karibu na wananchi ambapo wanajengewa uelewa mzuri kuhus masula mbalimbali ya kisheria na kupata ufumbuzi,” amesema

Kampeni hiyo inataratibiwa na serikali zote mbili kupitia wizara zinazoshughulika na katiba na sheria.

Amesema kauli mbiu ya awamu ya pili ya kampeni hiyo ni “msaada wa kisheria kwa haki, usawa amani, na maendeleo’ inayodhihirisha dhamira ya serikali kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa usawa kuimarisha amani katika jamii na kuweka msingi imara wa maendeleo.

Kwa mujibu wa Haroun, kaati ya wanufaika hao wanume walikuwa 213,723 na wanawake walikuwa 209,185 ambapo watu 4,971 walisaidiwa katika usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya Nida, huku migogoro 749 ilipokewa abapo migogoro 259 ilitatuliwa na 490 bado inaendelea kufuatiliwa.

“Mafanikio hayo yameonesha umuhimu wa kampeni hiyo katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu utatuzi wa changamoto mbalimbali za kisheria za kisheria zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.

Katika kampeni hi ya pili inalenga kutoa huduma zinazohusu masuala ya ndoa, talaka, mirathi, wosia na migogoro ya ardhi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuptiwa ufumbuzi wa changamoto zao.

Nao baadhi ya wananchi walionufaika na kampeni hiyo wameeleza umuhimu wake wakiwasshi wenye changamoto mbalimbali z akisheria kufika ili zipatiwe ufumbuzi.

Najim Haji Ali mmoja wa wanufaika wa kampeni hiyo amesema alikuwa na mgogoro wa ardhi katika Mkoa wa Kaskazini lakini baada ya kufikisha changamoto hiyo mbele ya wataalmu wa kempeni hiyo walipatiwa ufumbuzi hivyo akapongeza na kutaka wengine wapatiwe ufumbuzi.

“Ukiangalia maiaha ya wnanchi wengi ni masikini uwezo hawana masula ya kisheria yana gharama kubwa kwahiyo kupitia kapmeni hiyo wengi wanasaidiwa maana ni bure,” amesema

Naye Rajab Mzee Rajab amesema wanakabiliwa na migogoro ya mirathi kwahiyo anaamini baada ya kampeni hii kuanza atatumia fursa hiyo kuhakikisha wanapata ufumbuzi.