Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uokoaji kuendelea kumsaka aliyejirusha baharini Z’bar

Muktasari:

  • Uokoaji wa kijana aliyejitosa baharini jana Zanzibar umegonga mwamba katika siku ya kwanza kutokana na hali mbaya ya hewa, huku Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) ikisema itaendelea leo Jumatatu Januari 22, 2023.

Unguja. Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 amejirusha kutoka kwenye boti ya Zanzibar 3 na kuzama baharini huku jitihada za uokoaji zikigonga mwamba.

Tukio hilo limetokea jana Jumapili Januari 21, 2024 katika boti hiyo iliyokuwa ikitokea Pemba kwenda Unguja na kisha kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Sheikha Ahmed Mohammed akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu Januari 22, 2024  amesema mtu huyo baada ya kujitupa majini, boti ilizunguka mara tatu kumtafuta lakini ilishindikana kumpata.

Amesema mbali na boti hiyo kushindwa, walitumia vyombo vingine na boti za wavuvi kumsaka, lakini kutokana na hali ya hewa kwa mbaya walishindwa kumpata mtu huyo ila bado jitihada zaidi za kumtafuta zinaendelea.

“Kama tulivyoona kaanguka na watu walijaribu kumtafuta lakini hawakumuona, changamoto kubwa ni hali ya hewa kama tunavyoona siku hizi mbili hali ya hewa haikuwa nzuri na upepo mkali," amesema Sheikha

Bosi huyo wa ZMA amesema suala la uokozi ni la kitaifa na wadau wote hivyo wanaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha mtu huyo anapatikana.

Sheikha amesema wataendelea leo kumtafuta mtu huyo ili kuona kama wataweza kumpata kwani kuna wadau wengi wakishirikisha wavuvi yanapotokea matatizo kama hayo wanashirikiana nao.

“Mtu huyo (aliyejirusha) alikuwa na ndugu yake ambaye pia alipofika bandarini aliripoti kuwa ndugu yake alikuwa na changamoto ya akili,”amesema.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Khalid Salum Muhamed amesema baada ya jitihada za uokozi jana kushindikana, leo  wataendelea kumsaka kijana huyo.

"Taarifa nilizonazo kwabsasa jitihada zinaendelea baada ya jana kushindikana, nitatoa taarifa nyingine baadaye zitakazotokea,”amesema Waziri Dk Khalid.

Ofisa Habari wa Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) Ahmada Ahmada amesema kikosi hicho kitaendelea na jitihada za uokozi wakati wowote leo.