MATUKIO BUNGENI APRILI 3,2019





Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko akitoka kwenye ukumbi wa Bunge baada kuamriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoka ukumbini kufuatia kupiga kelele wakati spika alipokuwa akitangaza madeni aliyonayo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (kushoto) akizungumza na wabunge wenzake wa kambi ya upinzani baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuagia mbunge huyo kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Maadili, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza bungeni alipokuwa akiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema kuhusu uamuzi wake wa kuunga mkono kuwa bunge ni dhaifu huku akianika hadharani madeni ya mbunge huyo, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akijibu swali bungeni kuhusu changamoto zilizopo katika kushughulikia kesi za matukio ya unyanyasaji wa watoto, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akijibu swali bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kwa wanaume wanaotelekeza watoto wao hapa nchini, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi