Ramaphosa alivyosubiri urais kwa miaka 22

Muktasari:

  • Matamela Cyril Ramaphosa (65) amevuka vikwazo vingi kikiwemo cha kufungwa jela, kujitoa siasa lakini sasa ni Rais wa Afrika Kusini.

Baada ya kuongoza mchakato wa mazungumzo kati ya chama cha African National Congress (ANC) na serikali ya kibaguzi Afrika Kusini uliohitimishwa kwa utawala wa wazungu wachache kukabidhi kwa amani mamlaka kwa mpigania uhuru mashuhuri Nelson Mandela, Cyril Ramaphosa alianza kuwa na matarajio makubwa.

Akiwa Katibu Mkuu wa ANC (1991-1996), Ramaphosa alitamani urais. Matarajio yalikatika mwaka 1996 baada ya Thabo Mbeki kuteuliwa kuwa Naibu Rais wa Mandela kuchukua nafasi ya Frederik Willem de Klerk. Mwaka 1997 akajiuzulu siasa akahamia sekta binafsi, ingawa aliendelea kujihusisha na ANC.

Matumaini yalifufuka mwaka 2012 alipoteuliwa kuwa Naibu Rais katika ANC chini ya mkuu wa chama Jacob Zuma na mwaka 2014 alipanda alipoteuliwa kuwa Naibu au Makamu wa Rais wa Zuma.

Ndoto yake ilitimia Alhamisi ya Februari 15 baada ya kuteuliwa na wabunge na kuapishwa siku hiyo hiyo baada ya Rais Zuma kujiuzulu Jumatano usiku akiridhia shinikizo la chama kumtaka ang’atuke. Ni rais wa tano mweusi baada ya Mandela (1994-1999), Mbeki (1999 – 2008), Kgalema Motlanthe (2008-2009), na Zuma (2009-2018).

Safari ya maisha yake

Safari yake ya maisha ilianza Novemba 17, 1952 alipozaliwa akiwa mtoto wa tatu kwa mama Erdmuth na baba Samuel Ramaphosa – polisi mstaafu. Alizaliwa katika kitongoji cha Soweto, Johannesburg; alisoma Shule ya Msingi ya Tshilidzi na Sekano Ntoane High School na mafunzo kutoka Shule ya High School ya Mphaphuli huko Sibasa, Venda.

Baadaye aliingia Chuo Kikuu cha Kaskazini (Turfloop) mwaka wa 1972 ambako alisomea sheria na huko alijihusisha na harakati za siasa za wanafunzi.

Chuoni alikamatwa mara mbili miaka ya 1970 na kufungwa na serikali ya kibaguzi. Mfano mwaka 1974 alitumikia kifungo cha miezi 11 jela akiwa katika chumba cha peke yake lakini baadaye akawa karani katika kampuni ya sheria Johannesburg ambako alikamilisha masomo yake ya kisheria kupitia elimu kwa njia ya posta (Unisa).

Baada ya kuhitimu, aliingia kwenye vyama vya wafanyakazi - mojawapo ya njia za kisheria za kupambana dhidi ya serikali ya weupe wachache.

Kisha alijiunga na Baraza la Vyama vya Wafanyakazi wa Afrika Kusini (CUSA) akiwa mshauri katika idara ya kisheria ambako baadaye aliombwa aanzishe tawi la wafanyakazi wa mgodi. Mwaka 1982 alianzisha Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (NUM).

Mwaka 1985 NUM ilijiondoa CUSA na akashiriki kuanzisha Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (COSATU). COSATU iliunganisha nguvu na chama cha siasa cha United Democratic Front (UDF) dhidi ya serikali ya P. W. Botha. Mwaka 1987 Ramaphosa aliongoza mgomo mkubwa, ambao ulitikisa misingi ya uchumi wa enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi.

Majukumu ndani ya ANC

Mandela alipoachiwa mwaka 1990 baada ya kutumikia miaka 27 gerezani kwa kupinga ubaguzi wa rangi, Ramaphosa alikuwa muhimili wa kamati iliyopewa jukumu la kuongoza mabadiliko kuelekea kwenye demokrasia. Aliongoza kamati ya mapokezi ya Mandela kutoka gerezani na aliongozana naye katika safari ya Zambia.

Mwaka 1991 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa ANC. Aliinuka na kufahamika kimataifa kama mjumbe wa kuongoza mashauriano ndani ya ANC, na mchango wake ulionekana kuwa kiini cha mafanikio katika mazungumzo yaliyowezesha makabidhiano ya utawala kwa amani mwaka 1994.

Pia alishiriki kuandaa katiba mpya ya baada ya ubaguzi wa rangi, iliyoonekana kuwa moja ya katiba zinazotoa uhuru mkubwa ulimwenguni.

Mandela wakati fulani alimwelezea Ramaphosa kama mmoja wa viongozi wengi wenye vipawa katika “kizazi kipya” - wanaharakati vijana ambao waliongezeka katika miaka ya 1970, wakijaza nafasi iliyoachwa na wazee wao waliofungwa.

Lakini matumaini yake ya kupakwa mafuta kuwa mrithi wa Nelson Mandela yalipotea baada ya kuteuliwa Thabo Mbeki katika mbio za kuwa Naibu wa rais wa Afrika Kusini chini ya Mandela.

Miaka michache baadaye, Ramaphosa alijiondoa katika siasa na kuingia sekta binafsi. Kampuni yake ya Shanduka ilinunua hisa katika makampuni ya madini, simu na kampuni za McDonald na Coca Cola. Kufikia mwaka 2015 utajiri wake ulikuwa zaidi ya dola za Marekani 580 milioni.

Desemba 2007 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na mwaka 2012 alichaguliwa kuwa naibu wa rais katika ANC.

Mwaka 2014 baada ya kuteuliwa makamu wa rais aliamua kujiweka kando kwenye uongozi wa kampuni ili kuondokana na mgongano wa maslahi.

Kashfa dhidi yake

Kwanza alishutumiwa kwa kukaa kimya chini ya utawala wa Zuma. Wakosoaji walidai kuwa nafasi yake katika uongozi wa ANC ilimsaidia kupata taarifa za ndani.

Wengine walidai alikuwa na mkono katika mauaji makubwa yaliyofanywa na polisi tangu ulipokomeshwa utawala wa wachache mwaka 2012, polisi walipoua wafanyakazi 34 katika mgodi wa Marikana. Kipindi hicho Ramaphosa alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya kimataifa ya Lonmin ambayo ilikuwa inamiliki mgodi huo.

Pili alilaumiwa kwa kuwa upande wa menejimenti dhidi ya wafanyakazi wakati barua pepe zilipojitokeza zikimwonyesha wakihusisha na migomo ya wachimbaji kwamba amejiingiza katika “vitendo viovu vya uhalifu.”

Kamati iliyoongozwa na I.G. Farlam ilijikita kuchunguza kama menejimenti ya Lonmin iliihimiza serikali na polisi wapelekwe maofisa wengi kwenye mgodi huo na pia kuelezea kile kilichofanyika kama uhalifu dhidi ya maandamano ya wafanyakazi.

“Tume ilikuwa na maoni kwamba haiwezi kusema kwamba Ramaphosa alikuwa ‘sababu ya mauaji’,” ripoti hiyo ilisema. “Hakuna msingi wowote kwa tume kumhusisha na kumwona Ramaphosa kuwa na hatia ya makosa ambayo anadaiwa kufanya.”

Baadaye Ramaphosa aliomba radhi kupitia redio ya taifa ili kuokoa uadilifu wake katika ANC na umoja wa wachimbaji.

Katika uchaguzi wa rais wa ANC Ramaphosa aliimarisha kampeni zake kwa kuelezea mapambano dhidi ya rushwa, ambazo zilimfanya awe kipenzi cha watu wa daraja la kati, wapigakura wa vijijini na viongozi wa wafanyabiashara.

Mara baada ya Ramaphosa kuwa rais wa ANC, shinikizo lilianza ndani ya chama kumtaka Zuma aondoke na amwachie nafasi hiyo naibu wake. Vikao vya ngazi ya juu vilifanyika na vilituma ujumbe kwa Zuma kwamba ajiuzulu.

Zuma alikataa kujiuzulu lakini tangazo lake la Jumatano usiku kwamba aliamua kuachia nafasi yake ya urais akitii uamuzi wa chama kumtaka ajiuzulu lilimtengenezea Ramaphosa njia ya kurithi kiti hicho alichokiota miaka 22 iliyopita.

Tatu mwaka 2017 alishutumiwa kwa kujihusisha na mapenzi na mabinti kadhaa lakini alikanusha.

Alikiri baadaye kwamba ni kweli alikuwa na mwanamke nje ya ndoa lakini aliviambia vyombo vya habari kwamba alimjulisha mkewe suala hilo.

Baadhi ya watu waliona kuwa kufichuka ghafla kwa suala hilo zilikuwa kampeni chafu za washirika wa Zuma ambao walikuwa wanamuunga mkono mgombea mwingine kuelekea uchaguzi mkuu – mtalaka wake Nkosazana Dlamini-Zuma.

Ramaphosa ana watoto wanne.

shfa hiyo hayakuu, Ramaphosa aliimarisha kampeni zake katika ujenzi wa uchumi wa nchi, kuongeza ukuaji na kubuni nafasi nyingi za kazi zinazohitajika.

Matarajio

Ramaphosa ambaye kwa kiasi kikubwa anaonekana kuwa mjuzi wa biashara, anasubiriwa kusaidia uimarishaji ustawi wa kisiasa na kusaidia kushawishi uwekezaji kwa Afrika Kusini.

Kashfa dhidi yake

Lakini alishutumiwa kwa kukaa kimya chini ya utawala wa Zuma. Wakosoaji walidai kuwa nafasi yake katika uongozi wa ANC ilimsaidia kupata taarifa za ndani.

Wengine walidai alikuwa na mkono katika mauaji makubwa yaliyofanywa na polisi tangu ulipokomeshwa utawala wa wachache mwaka 2012, polisi walipoua wafanyakazi 34 katika mgodi wa Marikana. Kipindi hicho Ramaphosa alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya kimataifa ya Lonmin ambayo ilikuwa inamiliki mgodi huo.

Alilaumiwa kwa kuwa upande wa menejimenti dhidi ya wafanyakazi wakati barua pepe zilipojitokeza zikimwonyesha wakihusisha na migomo ya wachimbaji kwamba amejiingiza katika “vitendo viovu vya uhalifu.”

Kamati iliyoongozwa na I.G. Farlam ilijikita kuchunguza kama menejimenti ya Lonmin iliwahimiza serikali na polisi kwanza wapelekwe maofisa wengi kwenye mgodi huo na pili kuelezea kile kilichofanyika kama uhalifu dhidi ya maandamano ya wafanyakazi.

“Tume ilikuwa na maoni kwamba haiwezi kusema kwamba Ramaphosa alikuwa ‘sababu ya mauaji’,” ripoti hiyo ilisema. “Hakuna msingi wowote kwa tume kumhusisha na kumwona Ramaphosa kuwa na hatia ya makosa ambayo anadaiwa kufanya.”

Baadaye Ramaphosa aliomba radhi kupitia redio ya taifa ili kuokoa uadilifu wake katika ANC na umoja wa wachimbaji.

Katika uchaguzi wa rais wa ANC Ramaphosa aliimarisha kampeni zake kwa kuelezea mapambano dhidi ya rushwa, ambazo zilimfanya awe kipenzi cha watu wa daraja la kati, wapigakura wa vijijini na viongozi wa wafanyabiashara.

Mara baada ya Ramaphosa kuwa rais wa ANC, shinikizo lilianza ndani ya chama kumtaka Zuma aondoke na amwachie nafasi hiyo naibu wake. Vikao vya ngazi ya juu vilifanyika na vilituma ujumbe kwa Zuma kwamba ajiuzulu.

Zuma alikataa kujiuzulu lakini tangazo lake la Jumatano usiku kwamba aliamua kuachia nafasi yake ya urais akitii uamuzi wa chama kumtaka ajiuzulu lilimtengenezea Ramaphosa njia ya kurithi kiti hicho alichokiota miaka 22 iliyopita.

Maisha ya ndoa

Ramaphosa ana watoto wanne kwa mke wake wa pili Tshepo Motsepe, ambaye ni daktari.

Mwaka 2017 alishutumiwa kuwa alikuwa akijihusisha na mapenzi na mabinti kadhaa lakini alikanusha.

Ramaphosa alikiri baadaye kwamba ni kweli alikuwa na mwanamke nje ya ndoa lakini aliviambia vyombo vya habari kwamba alimjulisha mkewe suala hilo.

Baadhi ya watu waliona kuwa kufichuka ghafla kwa suala hilo zilikuwa kampeni chafu za washirika wa Zuma ambao walikuwa wanamuunga mkono mgombea mwingine kuelekea uchaguzi mkuu – mtalaka wake Nkosazana Dlamini-Zuma.

Madhara ya kashfa hiyo hayakudumu, Ramaphosa aliimarisha kampeni zake katika ujenzi wa uchumi wa nchi, kuongeza ukuaji na kubuni nafasi nyingi za kazi zinazohitajika.

Matarajio

Ramaphosa ambaye kwa kiasi kikubwa anaonekana kuwa mjuzi wa biashara, anasubiriwa kusaidia uimarishaji ustawi wa kisiasa na kusaidia kushawishi uwekezaji kwa Afrika Kusini.