Mawaziri wakuu wastaafu waongoza kumuaga mke wa Kingunge

SEHEMU YA SHUGHULI ZA MAZISHI YA MKE WA KINGUNGE

Muktasari:

Peras Ngombale alifariki dunia Januari 4, mwaka huu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ugonjwa wa kupooza.

Dar es Salaam. Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba, Frederick Sumaye na Edward Lowassa wameungana na mamia ya ndugu, jamaa katika tukio la kuaga mwili wa mke wa Mzee Kingunge Kombale Mwiru.

Peras Ngombale alifariki dunia Januari 4, mwaka huu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ugonjwa wa kupooza.

Tukio la kuaga mwili huo leo Alhamisi limetanguliwa na matukio ya pole kwa familia ya mzee Kingunge.

Baada ya tukio zima la kuaga hapo nyumbani, mwili huo utapelekwa katika kanisa la Mtakatifu Peter kwa ajili ya ibada Maalumu kabla ya kuelekea Makaburi ya Kinondoni.