Watanzania kutembelea nchi 80 pasipo kuwa na viza

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema hayo leo (Jumatatu) bungeni alipojibu swali la mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kufahamu nchi hizo.

 Serikali imesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea bila kuhitaji viza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema hayo leo (Jumatatu) bungeni alipojibu swali la mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kufahamu nchi hizo.

"Zipo nchi 16 Afrika na 67 duniani ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea bila kuwa na viza," amesema Masauni.

Licha ya nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini), alizitaja zingine kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone na Togo ambazo hutumia mfumo wa viza on arrival.