Idadi ya Watanzania wanaotembelea vivutio vya utalii nchini inaongezeka

Thursday January 11 2018

 

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi [email protected]

Wakati juhudi zikifanywa kuongeza vivutio vya utalii kutoka hifadhi za Taifa ili kujumuisha vivutio vya asili pamoja na utamaduni, idadi ya watalii wa ndani inazidi kuongezeka.Baada ya hifadhi 16 zilizopo nchini chini ya usimamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kuonyesha mafanikio, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Chama cha wamiliki wa Mabasi Tanza-nia (Taboa) imeanza kuvitangaza vivutio vilivyopo kanda ya kusini.

Mpango huo unaolenga kuifungua kan-da ya kusini kutokana na vivuito vingi vya asili ilivyonavyo unahamasisha wananchi kufahamu maliasili zilizopo na umuhimu wake kiasi cha kuvuta wageni kutoka mbali na kuwahamasisha kuvitembelea kila watakapo kuwa na wasaa wa kufanya hivyo.

Juhudi hizo zinafanywa wakati mikakati ya kuzitangaza hifadhi 16 zenye ukubwa wa kilometa 57,024 za mraba pamoja na vivutio vinginemfano Mlima Kilimanjaro nje ya nchi zikiendelea. Kati ya hifadhi hizo, kumbukumbu zinaonye-sha, Serengeti iliyoanzishwa mwaka 1951 ndio kongwe zaidi.Hayo yote yakifanyika, kwa miaka miaka mingi idadi kubwa ya watalii wanaotem-belea vivutio vilivyopo nchini walikuwa wageni kutoka Amerika, Ulaya, Asia na Australia huku wanaotoka nchi nyingine za Afrika na wazawa wakiwa wachache hali ambayo imeanza kubadilika baada ya hamasa kuongezeka.Takwimu za hivi karibuni za Tanapa zin-aonesha mabadiliko makubwa ya watalii wanaotembelea hifadhi hizo kwani idadi ya watalii wa ndani inazidi kuongeezeka kila kukicha.Miongoni mwa sababu zinazotajwa ni mwamko wa Watanzania kuona umuhimu wa kutembelea hifadhi za taifa baada ya matangazo na uhamasishaji ambao ume-kuwa ukifanywa na mamlaka husika ikiwa-mo Tanapa, TTB na wadau wengine mmo-jammoja wakiwamo viongozi wa Serikali.TanapaTaarifa za Hifadhi ya Taifa Mkomazi iliyopo Wilaya ya Same mkoani Kiliman-jaro zinaonyesha kati ya mwaka 2009 hadi 2017, watalii 13,433 walitembelea kivutio hicho. Kati yao, watalii 8,445 walikuwa wa ndani huku 4,988 wakitoka nje. Ofisa utalii mwandamizi wa Mkomazi, Pellagy Marandu anasema utalii wa ndani una nafasi kubwa ya kushamiri kwa sababu ni wa gharama nafuu ukilinganisha na wanaotoka nje.Anasema ongezeko hilo limechangiwa na mwamko wa wananchi hasa wanafunzi wa vyuo, shule za sekondari na msingi na taasisi za umma na binafsi.


 Marandu anasema ni rahisi kwa wanaotaka kutembelea hifadhi hiyo iliyopo kilometa sita kutoka Mji wa Same kwa wanaofanya safari za kutwa hata wanaotaka kuwepo kwa zaidi ya siku moja kwani wanaweza kulala kwenye nyumba za wageni zilizopo mjini hapo au kutumia mahema yaliyopo ndani ya hifadhi hiyo.

Hali iliyopo Mkomazi inashuhudiwa Hifadhi ya Taifa Tarangire pia. Ofisa utalii mwandamizi wa Tarangire, Theodora Aloyce anasema awali wananchi walikuwa na hofu wakidhani gharama ya kutembelea hifadhi za taifa ni kubwa kutokana na kutokuwa au kuwa na taarifa ambazo si sahihi.

“Hifadhi zetu karibu zote unaweza kuja na gari lako binafsi ukalipia Sh11,800 kwa mtu mzima na Sh2,000 kwa watoto wenye miaka mitano hadi. Walio chini ya miaka mitano hawalipi,” anasema.

Anasema katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka, kuanzia Desemba 18 hadi 24, 2017 jumla ya watalii 1,890 wa ndani wametembelea hifadhi hiyo wakilinganishwa na 1,083 waliofanya hivyo kipindi kama hicho mwaka 2016.

Theodora, ambaye ni mkuu wa Idara ya Utalii Tarangire anatoa wito kwa wadau kuwekeza kwenye usafirishaji watalii wa ndani ili kuwezesha wananchi wanaotaka kutalii kufika kwa urahisi maeneo yao.

Anato mfano wa kufunguliwa kwa Barabara ya Dodoma hadi Babati kupitia Kondoa kwamba kumewezesha baadhi ya wananchi wanaoendesha magari yao binafsi kutembelea hifadhi hiyo huku kukiwa na fursa ya ama kulala kwenye hoteli zilizo nje au ndani ya hifadhi.

Ofisa utalii wa Hifadhi ya Tarangire, Godfrey Mbona anasema eneo hilo ni nyumba ya tembo kwani inayo idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na hifadhi nyingine Afrika.

“Mbali ya makundi makubwa ya tembo, Tarangire kuna wanyamapori wengine wengi, miti ya mibuyu pia imeenea kila mahali bila kusahau Mto Tarangire ambao ndio uhai wa hifadhi hii,” anasema Mboma.

Kati ya watalii 388,105 walitembelea Hifadhi ya Serengeti mwaka 2013/14 wazawa walikuwa 200,277 wakiwamo watoto 8,194. Mwaka uliofuata, 2014/15 kulikuwa na watalii 372,920 huku wa ndani wakiwa 198,515. Na mwaka 2015/16 kulikuwa na watalii 208,582 wa ndani, idadi kubwa ikilinganishwa na 180,945 kutokana nje huku mwaka 2016/17 jumla ya waliotembelea hifadhi hiyo walikuwa 355,793 wakiwamo 138,875 wa ndani.

Ofisa utalii mwandamizi wa hifadhi hiyo, Susuma Kusekwa anasema kuna hoteli sita za kifahari zinazotoa huduma kwa wageni wan je na ndani pamoja na mahema 14 ya kudumu na 138 ya muda. Vilevile, anasema kuna eneo ambalo mtalii wa ndani anaweza kufunga hema lake kwa gharama nafuu.

Rose Jumbe, mstaafu serikalini alitumia mapumziko ya mwisho wa mwaka akiwa na watoto, wakwe zake pamoja wajukuu 22 katika hifadhi ya Taifa Manyara anasema ni sehemu nzuri kutembelea na si gharama kubwa.

Anasema wamepata malazi ndani ya hifadhi hiyo kwa gharama isiyozidi 20,000 ya chumba cha kulala kwa siku na kuwa kama mgeni anapenda kulala nje ya hifadhi zipo nyumba za kutosha.

Hata hivyo kilio cha wahifadhi nchini ni namna utalii wa wanyamapori unavyoweza kuwa endelevu iwapo utashi wa kisiasa hautaweza kuingilia kati kuokoa mapito ya wanyama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Mapito ya wanyamapori au ushoroba yameathiriwa kwa kiwango kikubwa na ongezeko la watu bila kuzingatia mipango bora ya matumizi ya ardhi limesababisha uanzishwaji wa mashamba pamoja na ujenzi wa makazi.

Mkuu wa idara ya utalii wa Hifadhi ya Taifa Arusha (Anapa), Neema Philipo anasema wanyapori wanapaswa kuwa huru kutoka hifadhi moja kwenda nyingine bila kikwazo lakini imekuwa tofauti na wamekua wakijitahidi kuwaelimisha wananchi kutoingilia ushoroba.

Lengo la kulinda mapito hao ni kuwawezesha kupata malisho sanjari na kuzaliana na kuepusha uzao wa aina moja unaotokana na wanyama wenye nasaba moja.

Kinapa

Wakati utalii wa hifadhi ukiongeza idadi ya watalii wa ndani wanaotembelea vivutio hivyo hali ni tofauti kwa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa) ambayo watalii wengi ni wageni kutoka nje ya nchi.

Ofisa utalii wa Kinapa, Herman Mtei anasema kwa miaka 10 iliyopita, jumla ya watalii 483,047 walipanda Mlima Kilimanjaro lakini wenyeji walikuwa 28,097 tu sawa na asilimia 5.82 ya walioutumia mlima huo.     

Advertisement