Kombinesheni za hawa usipime

Muktasari:

  • Wenyewe wanajua tu kwamba nani anafanya nini na nani wa kutupia katika mazingira yapi.

Mashabiki wakiingia uwanjani, cha kwanza walikuwa wakiangalia watu watatu hasa kule mbele, Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya.

Wenyewe wanajua tu kwamba nani anafanya nini na nani wa kutupia katika mazingira yapi.

Mechi ya juzi na Kagera, wapo waliooshangaa Bocco kuanzia benchi lakini ni mambo ya kocha anavyoamua. Simba ililala bao 1-0.

Okwi/Bocco

Hawa wawili waliibeba Simba kwa kiasi kikubwa. Pacha yao imeshatupia mabao 34.

Ilikuwa safu moja matata kuliko timu yoyote na kufanikisha kwa kiasi kukubwa kutwaa ubingwa.Okwi ndio kinara wa mabao amefunga 20 mpaka sasa huku Bocco akiwa wa pili na mabao 14. Ni wazi Okwi na Bocco ndizo pacha kali msimu huu zilizoibeba Simba.

Mlipili/Nyoni

Beki kiraka Erasto Nyoni ni miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa msimu huu.

Nyoni mwanzo wa Ligi alikuwa akicheza namba yoyote nyuma na sasa ana maelewano makubwa na chipukizi Yusuph Mlipili.

Mlipili amekuwa pacha na Nyoni katika nafasi ya ulinzi wa mabeki wa kati na kuruhusu mabao 14 likiwemo la Kagera Sugar juzi.