Mwanamke tajiri anayelea yatima 40,000

Muktasari:

Anasema kukata tamaa ni dhambi kwa sababu aliyewaona mwaka 1996 hawezi kuamini akiwaona sasa kwa sababu hakuwa na kitu zaidi ya kupata mlo mmoja kwa siku.

Wakati mwingine misukosuko hufungua njia kuelekea mafanikio. Hivyo ndiyo inavyoweza kuwa kwa mke wa bilionea wa Zimbabwe, Strive Masiyiwa, Tsitsi Masiyiwa alivyoanza hadi kufika alipo sasa.

Anasema kukata tamaa ni dhambi kwa sababu aliyewaona mwaka 1996 hawezi kuamini akiwaona sasa kwa sababu hakuwa na kitu zaidi ya kupata mlo mmoja kwa siku.

“Tulikuwa hivyo, hatukuweza kuwapa hata chai wageni walipokuja kututembelea, tulikuwa tunafanya kazi ili ya mkono uende kinywani, ”anasema Tsitsi alipokuwa kwenye mahojiano maalumu na jarida la Retrospect.

Anasema maisha hayakuwa hivyo siku zote, kwa sababu mumewe alijitahidi na kuanzisha kampuni ya kusambaza umeme ambayo ilipata mikataba mikubwa na kupata faida kutokana na kupata kazi nyingi za Serikali.

Anasema, misukosuko haikuisha kwani mwaka 1993, mumewe aliamua kuanzisha kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi , ambayo mshindani wake mkuu ingekuwa kampuni ya Serikali inayojishughulisha na shughuli kama hizo.

Anafafanua kuwa wakati huo kampuni pekee iliyokuwa ikitoa huduma ya mawasiliano nchini Zimbabwe ilikuwa ilikuwa Zimbabwe Post & Telecommunications Corporation (PTC).

“Tatizo letu lilianza alipoishitaki Serikali, Masiyiwa alidhani mahakama inatenda haki kumbe kuishitaki Serikali siyo kazi rahisi”.

Anaeleza madhara yaliyotokana na kuishitaki Serikali, jambo la kwanza walivunja mikataba yote na kampuni ya mumewe Retrofit iliyokuwa ikisambaza umeme.

“Niliweka agano na Mungu kama tungeshinda kesi hiyo iliyoturudisha kwenye umasikini uliotopea nitawasaidia masikini wenye mahitaji kwa maisha yangu yote,” anasema.

Walimtumainia Mungu pamoja na mumewe ikiwa ni pamoja na kuchukua uamuzi mgumu wa kusaidia wenye shida ilihali na wao wana shida

“ Mungu alijibu maombi kwa sababu Disemba 1997 Mahakama Kuu ya Zimbabwe ilitoa leseni kwa kampuni ya Econet Wireless ya kuanzisha huduma ya mawasiliano ya simu.”

Hatimae Econet ilizindua huduma zake nchini Zimbabwe mwaka 1998. Ukuaji ulikuwa wa haraka. Miaka 15 iliyopita imejitanua kwa kukusanya wanachama 10 milioni na kuenea kote nchini humo, Botswana, Burundi na Lesotho.

“Mimi nilikusanya yatima wengi na kuwasomesha, kuwasaidia, kuwatafutia wafadhili, bado natimiza ahadi niliyoweka kwa Mungu,” Tsitsi anasema.

Anasema amekuwa akitoa msaada kwa watoto anaoishi nao, kutembelea yatima katika vituo vyao na kutoa elimu ya kuwapa moyo na kuwaongezea kujiamini.

“Nilitumia muda na watoto hawa na nimekuwa upendo wao. Nilitaka kuendelea kufanya zaidi kwa ajili yao, lakini mimi kutambua kuwa ilikuwa haitoshi kuendelea kuwapa samaki. Nilikuwa na kuwafundisha jinsi ya kuvua samaki, “anasema.

Ni katika hatua hiyo kwamba Kafarnaumu Trust alianza kwa bidii, kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kulipa ada ya shule na kutoa fedha kwa ajili ya sare za shule na vifaa vya.

Anafafanua kuwa akaamua kufungua mfuko kwa ajili ya watoto hao, Kapernaumu, baada ya kuona haitakiwi kuwapa samaki bali kuwafundisha kuvua samaki, jambo pekee watakaloweza kufaidika nalo ni elimu.

“Leo mfuko wa Kapernaumu unalipa ada zaidi ya wanafunzi 40,000, ambao Tsitsi anawaita “Historia Makers,”.

Anasema kati ya wanafunzi hao 3, 000 wanasoma Chuo Kikuu na baadhi yao nchini Marekani, Afrika Kusini na Australia.

Amefurahishwa na kuamini akiweka hadi na Mungu kama una moyo inakuwa kwani Februari mwaka huu Tsitsi na mume wake wameanzisha mfuko wa elimu walioupa jina Balozi Andrew.

Anasema mfuko huo ni kwa ajili ya udhamini wa wanafunzi wa Afrika watakaopata nafasi ya kusoma Chuo kikuu nchini Marekani.

Anaeleza kuwa hata jina la mfuko huo ni kuonyesha heshima ya Balozi Andrew Young, Mmarekani aliyekuwa Balozi wa Umoja wa Mataifa, ambaye ni maarufu kutokana na juhudi zake za kupambania wengine.

Anasema mfuko huo kwa sasa upo nchini Zimbabwe, Burundi, Afrika Kusini, Lesotho na Swaziland, mpango wao ni kuongeza nchi nyingi zaidi.

Jarida la Forbes linamtaja mama huyu kama kinara na mkombozi wa watoto wa Afrika na maendeleo ya Bara hilo kwa ujumla na ni mwanzilishi mifuko mingine mitatu kama hiyo ikiwamo Christian Community Patnership Trust (CCPF), unaosaidia kueneza Injili maeneo ya vijijini nchini Zimbabwe, National Health Trust Of Zimbabwe ambayo unatoa msaada wa fedha kwa ajili matibabu na Joshua Nkomo Scholarship Fund. Huu ni kwa ajili ya kusaidia watoto wenye uelewa maalumu wa masomo.

Aprili mwaka huu alijiunga na wawekezaji wakubwa barani Afrika kama vile Nigeria mwekezaji Tony Elumelu, Kenya, James Mwangi na Nigeria, Toyin Saraki kuunda umoja unaoitwa African Philanthropy Forum (APF). Lengo la umoja huu ni kuunganisha Waafrika wenye uwezo na kushirikiana na wafadhili kusaidia maendeleo ya Afrika.

jina Balozi Andrew.

anapoweza alianzisha Asasi isiyo ya Kiserikali (NGo) ambayo inashughulikia masuala ya Kijamii katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini (Economic Growth and Social Welfare Foundation Gwrowth and Social Welfare-EGOSF.

Dondoo

Mulenda alizaliwa Januari 25, 1972, Biharamulo mkoani Kagera.

Mtumishi wa umma Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, katika nafasi ya ukaguzi wa mahesabu.

Mwaka 2015 aliwania pia nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhiri ya Muungano wa Tanzania.