Ni staa, ndinga na mjengo mkali, waleti inasoma... halafu bado dogo!

Muktasari:

Hivi umeshawahi kusikia Chama cha Wanaume? Umoja wa Wanaume? Umoja wa Wanasheria Wanaume? Umoja wa Madaktari Wanaume?

Kuwa mwanaume siyo mchezo na siyo lelemama. Achana na mtoto wa kiume au mvulana. Tunaongelea wanaume.

Hivi umeshawahi kusikia Chama cha Wanaume? Umoja wa Wanaume? Umoja wa Wanasheria Wanaume? Umoja wa Madaktari Wanaume?

Hii inamaanisha mwanaume ni taasisi inayojitegemea.

Mwanaume kamili aliyekamilika siyo kama wale wa kutoka Canada ambao wapo na walikuwepo kwa ajili ya kunyonya wanyonge.

Ili uwe mwanaume yakupasa kwanza kabisa kumshukuru Mungu kwa kuumbwa jinsia ya kiume.

Umepewa upendeleo lazima ushukuru. Halafu uwe rijali na mmiliki. Ukishakuwa rijali unapaswa uwe na umiliki.

Umiliki wa mwanaume rijali ni umiliki wa mwanamke/wanawake. Iwe rasmi au vinginevyo.

Umiliki wa watoto pia ni muhimu japokuwa hili linategemea zaidi mapenzi ya Mungu.

Ikumbukwe kuwa mwanamke ni mali ya mwanaume lakini watoto ni mali ya mwanamke na mwanaume.

Uwe na maamuzi. Usilegelege katika maamuzi yako. Mwanaume ndiyo kichwa cha familia, kichwa hakipaswi kuyumbishwa na mabega sawa? Kumbuka wewe ni taasisi!

Mwajibikaji. Uajibikaji ni wajibu wako kuhakikisha mwanamke unayemmiliki anatosheka na kuridhika na huduma zako.

Baiolojia yake ipate habari yake sawa sawa, tumbo lake lipate chakula cha kutosha, mwili wake upate mavazi na miguu ivishwe viatu.

Mkipata watoto na mwanamke wako ni wajibu wako kuhakikisha wanapata mahitaji yote wanayostahili.

Kama huna uwezo kwa nini uzae kama kuku?

Ukishafanikiwa kuyamudu yote hayo hapo juu, usisahau kuwa duniani kuna wanaume wenzako. Tafuta muda wa kukutana na wanaume wenzako uongeze ujuzi na maarifa ya kuishi kiume.

Hapo bia na nyama choma vinaruhusiwa kusikiliza maongezi yenu. Ukishapiga haya makitu rudi kwa mwanamke wako kampe haki yake amazing.

Ikumbukwe kuwahi kurudi nyumbani si sifa ya mwanaume. Mwache Mwanamke wako awe na muda wa kuwa huru na kulea watoto. Apige umbea na mashosti zake.

Inapotokea kwa namna yoyote na kwa sababu yoyote ile nafsi yako ikakosa umakini. Na kujikuta shetani anashika dimba la ubongo wako na kukumiliki atakavyo.

Na ukijikuta unaenda nje ya mwanamke wako, hakikisha akili yako inafanyakazi.

Kuna wakongwe wenzangu. Wanaume wenzangu kibao wako hata mtaani kwako wanaweza kuendeleza huo mlolongo kwa kukuelekeza mwanaume anatakiwa aishi vipi na mwanamke. .

Au kama vipi, leo ni Jumamosi, tunaweza kupanga mkakati wa kukutana ili tuzungumzie uanaume kama uanaume. Ili kupunguza masela wanaozeeka bila wake na wanaooa mapema na kushindwa kudumu na mwanamke.

Iko hivi. Mwanaume anaweza kuchepuka na bado akawa na upendo wa dhati kwa mke wake (ingawa sishauri), lakini mwanamke hawezi kuchepuka na akaendelea kumpenda mume wake kwa dhati.

Kwa sababu mwanaume hafanyi tendo la ndoa kwa hisia, mwanamke hawezi kufanya tendo la ndoa bila hisia.

Ndiyo maana wanaume wanahitaji mahali pa kufanyia tendo la ndoa ila wanawake wanahitaji sababu ya kufanya tendo la ndoa.

Wanawake wengi wanaoenda mahakamani kudai talaka kwa waume zao ni wale wachepukaji.

Mwanamke asiyechepuka hawezi kwenda mahakamani kudai talaka isipokuwa kama mumewe atakuwa amezidisha unyanyasaji wa kimwili na kiakili kiwango cha kukaribia kumuua mkewe.

Wanaume hawawezi kubadili tendo la ndoa na upendo. Mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa na mwanamke lakini bado akawa hampendi.

Lakini pindi tu mwanamke aliyeolewa anapolala na mchepuko wake huanza hata kusimulia habari za siri kuhusu mume wake, na anaweza pia kusema ni kwa namna gani anamchukia mume wake.

Kwa mwanaume tendo la ndoa na upendo ni vitu viwili tofauti kabisa, lakini kwa mwanamke tendo la ndoa na upendo ni vitu viwili vinavyoenda sambamba.

Kwa mwanaume tendo la ndoa huja kwanza kabla ya upendo lakini kwa mwanamke upendo huja kwanza kabla ya tendo la ndoa.

Pindi mwanamke anapoanza kuchepuka anakuwa ametumbukia kimapenzi kwa mchepuko huo na maisha kwenye ndoa hayawezi kuwa sawa kamwe.

Na anaweza hata kumuua mumewe endapo tu atakuwa ameanza kuchepuka. Mkeo akianza kuchepuka utakuwa mwanaume mwenye bahati sana endapo utaendelea kuishi kwa amani.

Tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya wanawake wanaochepuka huwaombea waume zao wafe haraka.

Ndiyo maana ni hatari sana kwa mwanaume kuendelea kuishi na mwanamke anayechepuka.

Inashauriwa kila mahali hata kwenye vitabu vitakatifu kumtaliki mwanamke pindi tu anapogundulika kuwa amezini.

Mwanamke hawezi kuchepuka na mtu ambaye hampendi, huwa wanaitoa mioyo yao kwa kila kitu. Ndiyo maana huwezi kuamini maamuzi yao.

Kichekesho kikitolewa wanawake wengi wanaocheka hawacheki eti kwa sababu kichekesho ni kizuri, ila ni kwa sababu huwapenda wale waliotoa vichekesho hivyo.

Na endapo hawakupendi hata kichekesho chako kingekuwa kizuri kwa kiasi gani hawatacheka.

Tafiti zinaonesha kuwa ndoa nyingi huanza kuyumba pindi mwanamke anapoanza kuchepuka.

Kuna wanaume wengi wanaochepuka lakini bado wanawaonesha wake zao upendo wa dhati.

Ila ni vigumu kukuta ndoa imesimama na mambo yanaenda sawa huku mwanamke akiwa mchepukaji.

Pindi mkeo anapoanza kulala na mwanaume/wanaume wengine ujue kifo chako kiko karibu kama kope na jicho.

Mwanadada wa Kiganda. Mzuri kwa maana ya uzuri. Zarina Hassan ‘The Bosslady’. Ameamua kujitenga na mbavu za Diamond Platinumz.

Wakati siku ya wapendao watu waliitumia kuimarisha mapenzi yao. Yeye katumia kukatisha penzi lake kwa baba wa watoto wake wawili.

Kashindwa kupambana na vurugu za kijana mdogo mwenye kila kitu kwenye maisha yake. Kijana anayeishi maisha ambayo kila kijana anatamani au kuyaota.

Shughuli za Diamond. Umaarufu wa Diamond. Pesa za Diamond. Umri wa Diamond. Na njaa za kina dada wa mjini. Ni vigumu sana kutulia.

Anahitajika mwanamke mwenye upungufu kidogo wa akili ili kuhimili presha hiyo. Diamond yupo kwenye kilele cha vilele vya mafanikio.