Chelsea, Man City zawekwa kikaangoni Fifa

Muktasari:

Hii inakuwa mara ya tatu kwa shirikisho hilo la soka kuichunguza  Chelsea ambayo mwaka 2009 ilizuiwa kufanya hivyo kwa miaka miwili.

England. Timu za soka za Chelsea na Manchester City zinachunguzwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusiana na namna zinavyowasajili wachezaji chipukizi.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa shirikisho hilo la soka kuichunguza  Chelsea ambayo mwaka 2009 ilizuiwa kufanya hivyo kwa miaka miwili.

Mwezi Mei, Bodi ya Ligi Kuu England iliitoza faini Man City ya Pauni 300,000 na kuifungia kusajili wachezaji wa akademi kwa miaka miwili.

Fifa imekuwa na msimamo mkali katika kusimamia usajili wa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 ili kulinda haki zao.