Jogoo, ABC, Pazi zatakata RBA -VIDEO
Muktasari:
Katika mchezo mwingine uliochezwa saa 2:00 usiku, Pazi iliichapa Chui kwa pointi 71 -48.
Hadi sasa mabingwa watetezi Savio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 22 wakifuatiwa na Vijana City Bulls wenye pointi 21 wakati Ukonga Kings ya tatu ikiwa na pointi 19.
Dar es Salaam. Jogoo imeifunga Mgulani kwa pointi 84-53, huku ABC ikichakaza TZ Prisons pointi 75-55 katika mchezo wa Ligi ya Mpira wa Kikapu inayoendela kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo mwingine uliochezwa saa 2:00 usiku, Pazi iliichapa Chui kwa pointi 71 -48.
Hadi sasa mabingwa watetezi Savio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 22 wakifuatiwa na Vijana City Bulls wenye pointi 21 wakati Ukonga Kings ya tatu ikiwa na pointi 19.
Sylvian Yunzu wa Savio ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga pointi nyingi akiwa amefunga pointi 195 hadi sasa akifuatiwa na Ally Hashim wa Ukonga Kings aliyefunga pointi 186 wakati Yassin Choma wa Kurasini Heat akiwa nafasi ya tatu kwa kufunga pointi 181.
Pia, Yunzu anaongoza kwa wachezaji mahiri wa kufunga kwa kutumia mitupo mitatu (Three pointi) akiwa amefunga mara 43 akifuatiwa na Erick Lugora wa Oilers aliyefunga mara 23 na Frank Majura wa ABC akifunga mara 22.