England yakomalia ubaguzi Russia

London, England. England imeanza kuchukua hatua kuhusu vitendo vya ubaguzi zinavyoweza kuwakumba wachezaji wa timu hiyo katika fainali za Kombe la Dunia.

Kocha wa England Gareth Southgate anatarajiwa kuteta na wachezaji hao ili kuwapa mbinu za kujilinda na ubaguzi kwenye mashindano hayo.

Southgate ameamua kuchukua tahadhari mapema kutokana na rekodi mbaya ya nchi za Russia na England katika medani ya soka.

Timu hizo zimekuwa na uhasama mkubwa na mashabiki wa pande hizo wamekuwa wakizichapa na timu zao zinapocheza katika mashindano mbalimbali.

Chama cha Soka England (FA), kimewataka wachezaji wa timu hiyo kuripoti haraka viashiria vya ubaguzi kwa mwamuzi au ofisa wa mchezo husika.

“Tutafanya kazi na wachezaji jinsi ya kuunga mkono kwa tukio lolote ambalo litampata mwenzao, moja ya hatua za kuchukua ni kufuata utaratibu kwa maofisa wa mchezo,”a lisema Southgate.

Kocha huyo alisema wachezaji watapewa mbinu na hatua muhimu za kuchukua wanapofanyiwa vitendo vya ubaguzi.

England na Ufaransa ndio waathirika wakubwa wa ubaguzi kwa kuwa timu zao zinaundwa na baadhi ya wachezaji wenye asili ya Afrika.

Timu hiyo inatarajiwa kufungua pazia la mashindano hayo kwa kuvaana na Tunisia Juni 18.