Thursday, September 14, 2017

Harmonize na Wolper bado balaa

 

By Frank Ngobile

Dar es Salaam. Hali inazidi kuwa kupamba moto baada ya majuzi msanii kutoka WCB, Harmonize kudondosha wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Nimechoka’ ambapo kwa udadisi wa ndani ni wimbo unaonekana kumlenga mpenzi wake wa zamani Jackline Wolper.

Kuonesha kwamba yeye Wolper si wa mchezomchezo, kupitia akaunti yake ya Instagram aliposti dongo zito kuelekea kwa Harmonize huku akizidi kumtuhumu yeye kuwa ndiye mdanganyifu wa mapenzi na si kama jinsi Harmonize anavyodai na baadaye akafuta posti hizo.

Baada ya dongo hilo Harmonize ameamua kujibu nae katika akaunti yake ya Instagram, ambapo aliposti video fupi akiwa na mpenzi wake mpya na kuandika maneno kadhaa.

“Vipi kwani? Mbona nasikia mtaa wa 3 povu kwani katajwa mtu? Meseji ikishafikaga..Ukweli unaumaga..??#Nimechoka mwambie tena anaejifanya anakujua sana…Pambana na huba lako.”

Baada ya mapovu ya wote wawili juhudi za kuwatafuta kila mmoja ili kuweza kuelezea jambo hilo linaloendelea zimegonga mwamba sababu hakuna anayepokea simu kujibu juu ya mapovu hayo.

 

-->