Thursday, September 14, 2017

Houdgson amnyemelea Wilshere

 

London, England.Kocha Roy Houdgson ameripotiwa kumtaka kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere katika usajili wa Januari.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England alikubali kuinoa Crystal Palace baada ya kutimuliwa kwa kocha Frank de Boer aliyeiongoza timu hiyo katika mechi nne za Ligi Kuu England msimu huu.

Gazeti la Daily Mail liliripoti kwamba Hodgson ana nafasi kubwa ya kumsajili Wilshere, ambaye sasa ana miaka 25, katika usajili wa Januari.

Hodgson mwenye miaka 70 atamwangalia kwa ukaribu kiungo huyo wa kimataifa wa England hadi mwaka mpya kabla ya kuamua kumsajili au vinginevyo.

Taarifa zinadai kuwa kama Wilshere atashindwa kuingia katika mipango ya kikosi cha kwanza cha kocha Arsene Wenger, atajaribu kumpeleka Selhurst Park.

-->