Milioni 177 zamng’oa Kichuya Simba

Muktasari:

  • Profesa Midundo alisema kuwa mbali na hilo wameangalia ofa ambayo nyota huyo amepewa ya dola 80000 (Sh177 milioni) ni kubwa kuliko ambayo atapewa na  Simba.

 

Kuna taarifa za chinichini zinaeleza kuwa winga wa Simba, Shiza Kichuya amegoma kusaini mkataba mpya klabuni hapo baada ya kupata ofa ya maana kutoka kwa timu moja ya Kiarabu.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji kadhaa ambao mikataba yao na Simba inaelekea ukingoni na mabosi wa timu hiyo tayari wameanza kuhaha kumshawishi aongeze kandarasi hiyo inamalizika mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo kiwango kilichoonyeshwa na winga huyo tangu ametua Msimbazi na pia katika michuano ya COSAFA iliyofanyika Afrika Kusini mwezi Julai, kimempa ulaji kutoka kwenye timu hiyo kutoka ukanda wa Afrika Kaskazini.

Meneja wa mchezaji huyo Profesa Midundo Mtambo amedokeza kuwa wanataka mchezaji huyo akacheze soka la kulipwa nje ya nchi kwani itakuwa faida kwake (Kichuya) na Taifa zima.