Man United, Chelsea zajisogeza kwa Lewandowski

Muktasari:

  • Timu za Chelsea na Manchester Unied zimejiweka wkenye mbio za kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich.

England. Timu vigogo za Ligi Kuu England zimeingia kwenye vita ya kimyakimya ya kutaka kufanya usajili wa Nyota wa a Bayern Munich Robert Lewandowski.

Taarifa zainaelezwa kwamba mchezaji huyo hana mpango wa kuendelea kuwapo Bayern Munich licha ya mkataba wake kuisha mwaka 2021.

Upepo wa kuondoka au kubaki kwa mchezaji huyo kutakolezwa na kasi ya wakala wake wa kujitegemea,  Pini Zahavi iwapo atafanikiwa kumshawishi.

Sky Sports ilienzwa kwamba suala la mchezaji huyo huenda likawekwa wazi wikimbili zijazo iwapo mipango itakwenda kama ambavyo ilipangwa.

Hivyo klabu za Manchester United na Chelsea zimeanza vita ya kimpya kimpya jambo hilo limevuta masikio ya mashabiki wa soka.