Mcha anoa makucha

Muktasari:

  • Ruvu inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi wenye timu 16 na ina pointi tano tu.

LICHA ya Ruvu Shooting, kuburuzwa mkiani kwenye msimamo wa ligi kuu, hakujamfanya straika wa timu hiyo, Khamis Mcha kukata tamaa,badala yake ameapa kuendelea kupambana hadi kieleweke.

Mcha alijiunga na Ruvu, akitokea Azam FC amesema, mahesabu yao ni kuona mechi zilizosalia kabla ya kuanza mzunguko wa pili zinawatoa mkiani.

"Tupo kwenye nafasi mbaya, lakini siyo sababu ya kutufanya tukate tamaa na kuona ndio mwisho wetu, tunaendelea kupambana kuona ni kwa namna gani tunaweza kuondoka mkiani kabla ya kuanza mzunguko wa pili,"alisema Mcha.

Amezungumzia nafasi yake ya kufunga na kwamba,  anaumiza akili kuona anafanikiwa kutimiza malengo yake ya kupachika mabao na kuisaidia klabu yake hiyo mpya.

"Kama mfungaji naumia pale ninapoona nakwama kutimiza wajibu wangu, lakini naendelea kupambana kuhakikisha nafanikiwa na mabosi wangu wafurahie huduma yangu,"alisisitiza Mcha.

Ruvu inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi wenye timu 16, ina pointi tano tu.