Neymar tunawasubiri nyumba Real

Muktasari:

PSG inahitaji kushinda 2-0 katika mchezo wa marudiano ili kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa

Madrid, Hispania. Baada ya kuonyesha kiwango kibovu, Neymar amesema Paris Saint-Germain haijakata tama katika kuhakikisha wanaitoa Real Madrid katika mchezo marudiano wa Ligi ya Mabingwa.

Mshambuliaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ametawala vichwa vya habari baada ya kuiongoza Real Madrid kushinda 3-1  kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu,  hata hivyo Neymar amesisitiza mechi ya marudiano Paris ndiyo itakayoamua.

"Hakuna kilichoamuliwa hadi sasa, bado kuna mechi ya marudiano," alisema nyota huyo wa Brazil.

Neymar pia alizima tetesi kuwa hana furaha ndani ya PSG, akipiga tetesi za yeye kuhusishwa na kutaka kuhamia Real mwisho wa msimu huu.

"Nina mkataba na PSG," alisema.

"Kwa sasa akili na mawazo yangu yote ni hapa PSG, Ninafuraha hapa."