Polisi Tanzania yaikamia Singida United

Muktasari:

Timu hiyo ya Polisi ilishindwa kupanda Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kufanya vibaya katika Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza

Arusha: Timu ya Polisi Tanzania imewasili Mkoani Singida tayari kwa mchezo wake wa Kombe la FA dhidi ya Singida United utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Kocha wa Polisi Tanzania, John Tamba alisema wamejiandaa kuibuka na ushindi katika mchezo huo kwa ndio mashindano pekee waliyosalia hivyo hawana budi kuhakikisha wanasonga hatua inayofuata.

“Tumesafiri na kikosi kizima tahari kwa mchezo huo kwakuwa hatuna majeruhi yoyote mpaka hivi sasa ndio maana ninajiamini tutapata matokeo,” alisema Tamba.

Aliongeza kuwa Singida ni timu kubwa na yenye uwezo mzuri katika ligi kuu Bara hivyo wanatarajia kupata ushindani katika mchezo huo lakini kwa maandalizi waliyoyafanya wanauhakika kupata matokeo mazuri.

Polisi Tanzania imesonga hatua hivyo baada ya kuitoa Friends Rangers kwa mabao 2-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Ushirika na sasa wanasaka ushindi wa kusonga hatua inayofuta.