Prisons yaitaka Simba ilipe dau la Mo Rashid

Muktasari:

  • Kauli ya viongozi hao wa Prisons imekuja wakati timu hizo inataraji kupambana kesho Jumatano katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Tanzania Prisons bado yaikomalia Simba juu ya usajili wa mshambuliaji wake Rashid Mohamed 'Mo' na kuwataka watimize kile walichokubalina.

Kauli ya viongozi hao wa Prisons imekuja wakati timu hizo inataraji kupambana kesho Jumatano katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa zinadai kuwa Simba ilimsajili Mo Rashid akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Prisons.

Akizungumzia sakata hilo Katibu wa Prisons, Havintishi Abdallah alismea kuna makosa yalifanyika, lakini tayari jambo hilo linafanyiwa kazi na kuwataka Simba watimize kile walichowaambia.

"Wakati mchezaji huyo anaenda kujiunga na Simba, uongozi wa Prisons ulimpa baraka zote na ndio maana hata jina lake halijapelekwa kuwa miongoni mwa wachezaji wetu kwa msimu wa 2018/19.

"Kuna fedha ambayo Simba tuliwaambia watulipe, ili kuuvunja mkataba huo, hivyo ni jambo ambalo linaendelea kufanyiwa kazi na siyo kwamba tumeliacha kama lilivyo ama kwamba linaweza kuibua mkanganyiko wowote la hasha,"anafafanua.