Samatta uso kwa uso na Pepe, azikwepa Arsenal, Chelsea
Muktasari:
- Safari ya kwenda Baku, Azerbaijan itakapochezwa fainali Mei mwakani imeanza rasmi baada ya kupangwa kwa makundi hayo leo.
Monaco, Ufaransa. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta atakuwa na kibarua kizito mbele ya beki mkongwe wa Ureno, Pepe baada ya Genk kupangwa Kundi I pamoja Besiktas, Malmo na Sarposborg katika mashindano ya Europa Ligi.
Mabao matano ya Samatta yameisaidia Genk kufuzu kwa hatua ya makundi, lakini sasa anategemea kupata upinzani mkali kutoka kwa Pepe anayesifika kwa kucheza soka la kibabe wakati Genk itakapowavaa Besiktas ya Uturuki inayopewa nafasi kubwa ya kumaliza kinara wa kundi hilo.
Nyota wengine wa Besiktas watakaowapa wakati mgumu Genk ya Samatta ni kiungo Mreno Ricardo Quaresma na Ryan Babel aliyewahi kutamba na Liverpool.
Mbali ya Besiktas pia Genk itakuwa na kibarua kutoka kwa timu za Scandnavia Malmo ya Sweden pamoja na Sarposborg ya Norway.
Samatta amesema hofu juu ya vigogo watakao kutana nao kwenye hatua hiyo ya makundi ambayo itaanza kuchezwa, Septemba 20.
Nahodha huyo wa Taifa Stars, amekuwa gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya kutokana na kiwango alichokionyesha kwenye michezo ya kuwania kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Safari ya kwenda Baku, Azerbaijan itakapochezwa fainali Mei mwakani imeanza rasmi baada ya kupangwa kwa makundi hayo leo.
Arsenal, Chelsea, Sevilla, AC Milan, Bayer Leverkusen na Lazio ni timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo.
Arsenal yenyewe ipo Kundi E pamoja na Sporting Lisbon (Ureno), Qarabag (Azerbaijan) na Vorskia (Ukraine).
Chelsea imetupwa Kundi L pamoja na PAOK (Ugiriki), Borisov (Bulgaria) na Vidi (Hungary).
Makundi
Kundi A: Leverkusen, Ludogorets, Zurich, Larnaca
Kundi B: Salzburg, Celtic, Leipzig, Rosenborg
Kundi C: Zenit, Copenhagen, Bordeaux, Slavia Prague
Kundi D: Anderlecht,Fenerbahce, Dinamo Zagreb
Spartak Trnava
Kundi E: ARSENAL, Sporting Lisbon, Qarabag, Vorskla Poltava
Kundi F: Olympiacos, Milan,Real Betis, Dudelange
Kundi G: Villarreal, Rapid Vienna, Spartak Moscow, Rangers
Kundi H: Lazio, Marseille, Frankfurt, Apollon
Kundi I: Besiktas, GENK, Malmo, Sarpsborg
Kundi L: CHELSEA, PAOK, BATE Borisov, MOL Vidi
Kundi K: Jablonec, Dynamo Kiev, Astana, Rennes
Kundi J: Sevilla, Krasnodar, Standard Liege, Akhisar