TFF watolea ufafanuzi pesa za Mtibwa Sugar

KATIBU mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wilfred Kidao amezitolea ufafanuzi pesa za bingwa wa kombe la Azam Federation Cup.

Tangu Mtibwa wawe mabingwa wa kombe hilo mwaka jana, baad ya kuifunga Singida Utd katika kombe hilo, hawakupewa zawadi yao huku taarifa zikiibuka kwamba Shirikisho hilo limepewa pesa na wamezitumia kwa matumizi mengine.

Kidao alisema kwamba amekuwa akishangazwa na maneno yanayosambaa kuhusu kutajwa Shirikisho hilo limepokea pesa za mshindi wa kombe la Azam Federation Cup na wamezitumia kwa matumizi mengine.