Simba kamili kuikabili Yanga

Muktasari:

  • Beki huyo amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeruhi

 Beki wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesema ilikuwa lazima waifunge Njombe Mji ili kupata morali ya ya kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Yanga wiki ijayo.

Simba na Yanga zitakutana Oktoba 28 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Hussein alisema walipambana ili kupata matokeo hayo kwani ushindi huo umewaongezea kasi ya kuivaa Yanga kikamilifu.

"Tumecheza vizuri dhidi ya Njombe Mji na ndio maana tukapata ushindi huo na ukiangalia tulistahili kupata ushindi mkubwa zaidi.

"Kilichowaponza wapinzani wetu ni kwamba walikuja kwa lengo la kujilinda zaidi hivyo kutupa wakati mgumu mwanzo, lakini baadae tukagundua na kubadilisha staili ya uchezaji na kupata ushindi," alisema.

Hussein alisema wanakwenda kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

"Mashabiki waendelee kuisapoti timu na sisi hatutawaangusha katika mchezo huo," alisema Tshabalala