Viera kumrithi Wenger Arsenal

Muktasari:

Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal kwa sasa anafundisha soka Marekani

London, England. Nguli wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira anatarajiwa kurejea katika kikosi hicho akiwa kocha mkuu.

Nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo na Ufaransa, anahusishwa na mpango wa kutua Emirates kujaza nafasi ya Arsene Wenger.

Mfaransa huyo alicheza kwa kiwango bora Arsenal kwa miaka tisa na alikuwa kipenzi cha kocha huyo.

Wenger anatarajiwa kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, baada ya kushindwa kuipa mafanikio muda mrefu.

Hata hivyo, Wenger atabaki katika klabu hiyo akiwa ni mmoja wa vigogo watakaokuwa katika benchi la ufundi.

Nguli huyo mwenye miaka 41, kwasasa anafundisha timu ya New York City baada ya kupata uzoefu katika benchi la ufundi alipojiunga na klabu ya Manchester City.

Kocha huyo anatajwa kuwa ni mmoja wa wachezaji bora wa kiungo waliowahi kutamba katika kikosi cha Arsenal na Ufaransa.