Friday, September 22, 2017

Wanamichezo kunufaika teknolojia mpya ya malipo

 

Dar es Salaam. Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya michezo hapa nchini leo imezindua mfumo kwenye simu za mkononi ili kusaidia wanamichezo  watoa huduma mbalimbali kufanya malipo.

Pia huduma hiyo itawawezesha wapenda michezo kushuhudia michezombali kwa kulipia gharama za ving’amuzi kupitia kutumia simu zao za mkononi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee alisema Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboresha zaidi.”

 

-->