Wabaya wa Yanga waweka Kambi Kariakoo
Muktasari:
- Yanga inaliwakilisha Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika CAF mchezo wa kwanza utakaopigwa dhidi ya St. Louis ya Shelisheli.
Kikosi cha St Louis ambacho kinashuka dimbani Jumamosi dhidi ya wenyeji Yanga, kimefanya mazoezi yake leo Jumatano kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam
Yanga inaliwakilisha Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika CAF mchezo wa kwanza utakaopigwa dhidi ya St. Louis ya Shelisheli.
Timu hiyo ya visiwani, imewasili jana Jumanne usiku na leo asubuhi wamefanya mazoezi uwanja wa Karume. Chanzo cha taarifa kilieleza kwamba kikosi hicho kimewaka kambi yao Kariakoo.
Kikosi cha Yanga kinajianda na mchezo huo kwa ujasiri baada ya kufanya vyema mechi zake tatu za hivi karibuni za Ligi Kuu.