Simba, Yanga zapangiwa vibonde CAF

Muktasari:

  • Timu hizo zimenusurika kukutana na Waarabu na badala yake zitaanza na timu vibonde raundi ya kwanza.

 Timu za Simba na Yanga zimenusurika kukutana na timu ambazo zilikuwa zinahofiwa kuwa zingekuwa mwiba kwao hasa zile za Waarabu kwenye mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Yanga itakutana  na  St Louis mchezo ambao itaanzia nyumbani na baadaye kuifuta ugenini.

Nayo Simba itakutana na Gendarmerie ya Djiboute ambayo pia itaanzia nyumbani na kumalizia ugenini.

Simba inarejea kwa mara ya kwanza kwenye mechi za kimataifa tangu mwaka 2013 ikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga itacheza tena Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.