Mtakaochaguliwa TFF, simamieni maagizo muhimu

Muktasari:

  • Wale watakaofanikiwa kuwashawishi wapigakura, ndiyo ambao Jumamosi ijayo ya Agosti 12 huko Dodoma, watakaopewa ridhaa ya kuliongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne kama katiba yake inavyoeleleza.

Kampeni za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinaanza leo kwa wagombea wa nafasi mbalimbali kupita kwa wapigakura kunadi sera zao.

Wale watakaofanikiwa kuwashawishi wapigakura, ndiyo ambao Jumamosi ijayo ya Agosti 12 huko Dodoma, watakaopewa ridhaa ya kuliongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne kama katiba yake inavyoeleleza.

Hatua ya kampeni imefikiwa baada ya hatua kadhaa ikiwamo kuchukua fomu na kurejesha, usaili, mapingamizi na nyinginezo ambazo ziliongozwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Revocatus Kuuli, kukamilika.

Katika hatua hizo, wapo waliojiondoa wenyewe kwa sababu wanazozijua lakini wapo walioondolewa kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza kama ilivyokuwa kwa Rais anayemaliza muda wake, Jamal Malinzi ambaye hivi sasa anashikiliwa na vyombo vya dola kutokana na kesi inayomkabili.

Tunaamini kwamba katika kampeni hizo, ushawishi kwa wagombea kwa kwa wapigakura ndiyo utakaowapa kura. Katika hilo tunapenda kuwaasa waliopewa dhamana ya kuchagua kuhakikisha kwamba wanatupatia viongozi wa kweli wa mpira, watakaousimamia na kututoa hapa tulipo.

Wakati wa kampeni, tunawaomba wapigakura na hata wagombea kujikita katika mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu, itakayotuwezesha kufika katika ngazi mbalimbali za michuano ya kimataifa pamoja na kutoa vijana wengi watakaosambaa katika ligi za mataifa mbalimbali duniani jambo ambalo siyo tu litaitangaza Tanzania kimataifa, bali litasaidia katika ajira na kuongeza kipato cha familia na Taifa.

Lakini pia kumekuwa na tatizo kubwa la mwendelezo wa kiuongozi. Kila wanapokuja wapya hufuta mambo ambayo hayaonekani kwa mtazamo wao kwenda sawa, tunadhani hili halifai. Yapo mambo ambayo hayafai kuachwa na mojawapo ni maazimio ya Bagamoyo ambayo mengi yamewekwa kapuni, ikiwamo kila timu kuwa na kikosi cha vijana.

Si hilo tu, Julai 30, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kupitisha mambo mbalimbali ikiwamo mabadiliko ya kanuni za Ligi Kuu mojawapo ikiwa ni afya za wachezaji pamoja na mikataba wanayoingia na klabu na kusema katika msimu wa 2017/18, hakuna mchezaji atakayesajiliwa na kupewa leseni ya kumruhusu kucheza Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili kama hatakamilisha masharti makuu matatu kwa mujibu wa kanuni.

Masharti hayo ni kuwa na bima ya matibabu, kuidhinishwa afya yake na Kamati ya Tiba ya TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 18 (1) ya Ligi Kuu na kuwasilisha TFF mkataba wake wa maandishi kwa mujibu wa kanuni ya 69 (8) ya Ligi Kuu. Pia, kwa mujibu wa Kanuni ya 69 (8), Kamati ya Utendaji imekubaliana kwamba: “Mkataba wowote wa wachezaji, ambao haujasajiliwa na kuthibitishwa na TFF, hautatambuliwa.”

Hayo ni maazimio machache tunayoona ni muhimu kuendelezwa ambayo tunasema viongozi wapya wayasimamie.

Pamoja na ukweli kwamba utawala mpya huja na taratibu zake, lakini tunadhani kwamba si vyema kufuta kila azimio na uamuzi uliofikiwa na wajumbe halali waliotangulia hasa yale ya msingi kwa kisingizio kwamba utawala mpya na mambo mapya.

Tuna imani kuwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi watachagua viongozi wenye dira na mwelekeo chanya wa mpira wa Tanzania.