‘Tujihadhari ongezeko maji ya bahari’>

Wadau wa mazingira wametakiwa kuchukua hatua kukabili ongezeko la maji ya Bahari ya Hindi ili kupunguza athari zilizoanza kujitokeza maeneo ya pwani.

Taarifa ya katibu mkuu, ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Joseph Malongo iliyosomwa na mkurugenzi wa tathmini ya athari ya mazingira wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Fadhila Khatibu ilisema ripoti za wanasayansi zinaonyesha ujazo wa maji ya bahari umeongezeka kwa wastani wa sentimita 19 hivyo kuongeza kasi ya mmomonyoko wa fukwe. (Mwandishi Wetu)