Wednesday, April 18, 2018

CRDB kulipa gawio la Sh5 kwa kila hisa

 

Benki ya CRDB imepanga kulipa gawio la Sh5 kwa kila hisa yake ifikapo Juni 5 mwaka huu. Gawio hilo linalipwa baada ya benki hiyo kupata faida zaidi ya Sh51.7 bilioni mwaka uliopita.

Taarifa iliyotolewa na benki hiyo jana inasema gawio hilo litalipwa baada ya kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanawahisa utakaofanyika Mei 19. Katibu wa benki hiyo, John Rugambo alisema: “Gawio litalipwa kwa wanahisa kupitia akaunti zao za benki, M-Pesa, Airtel Money au Tigo-Pesa.” Uorodheshaji wa wanahisa kwenye daftari utafanyika Mei 16 mwaka huu. (Mwandishi Wetu)

-->