Duce waja na teknolojia mpya majiko ya mkaa

Muktasari:

  • Lengo la majiko ni kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuyatumia kwa gharama nafuu na kupunguza madhara ya magonjwa yanayosababishwa na moshi wa mkaa.

 Wataalamu wa Sayansi na Teknolojia kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) wameanzisha mkakati wa kutengeneza majiko ya kisasa yasiyo na athari kwa watumiaji.

Lengo la majiko ni kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuyatumia kwa gharama nafuu na kupunguza madhara ya magonjwa yanayosababishwa na moshi wa mkaa.

Mhadhiri mwandamizi wa chuo hicho, Dk Dativa Shilla alisema majiko hayo yatapunguza gharama za nishati na kuepusha uwezekano wa kupata maambukizi yatokanayo na moshi. “Tulifanya utafiti wa majiko ya mkaa, tumegundua mengi yana madhara kwa binadamu hasa mtumiaji,” alisema jana kwenye wiki ya maonyesho ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa chuo hicho.

Mkazi wa Dar es Salaam, Naomi Biteko alisema teknolojia hiyo itawasaidia kuondokana na maradhi.

(Hellen Nachilongo)