Huawei yaingiza toleo jipya sokoni

Muktasari:

Simu mpya ya GR5 2017 inapatikana kwenye maduka ya simu kwa Sh685000 na inapatikana katika rangi ya kijivu,dhahabu na fedha.

Dar es Salaam. Katika kukabiliana na ushindani unaondelea kuimarika kwenye soko la mawasiliano, kampuni ya simu za mkononi ya  Huawei Tanzania imeingiza sokoni simu mpya  iliyotengenezwa kwa teknolojia ya juu.

Simu hiyo iitwayo GR5 2017 inatajwa kuwa na  yenye kamera mbili zenye ubora mkubwa  katika upigaji picha.

Akizungumzia kuhusu ingizo hilo jipya  sokoni, Mkurugenzi wa kanda wa Kampuni ya Huawei,  Mark Ho amesema licha ya kuwepo ushindani mkali, biashara ya kampuni ya simu za smartphone inaendelea kukua kwenye soko la ndani.

Ho amesema simu ya GR5 2017 imetengenezwa kwa ajili ya wapenda teknolojia wanaotafuta simu ya kisasa ya bei nafuu.

"GR5 2017 ni simu ya kwanza kabisa katika soko la ndani la simu za aina ya smartphone yenye kamera mbili zenye nguvu katika orodha ya simu za kiwango cha kati," amesema.

Amesema mwaka huu kampuni hiyo imejipanga kuendelea kuboresha ubora wa bidha zake huku ikiweka kipaumbele kwenye kuongeza wigo wa usambazaji.