Gwajima azungumzia utekwaji wa Roma Mkatoliki

Mwanamuziki Roma Mkatoliki.

Muktasari:

  • Akizungumza kanisani kwake leo, Gwajima alisema  Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam ndiye anayejua alipokuwa mwanamuziki Roma Mkatoliki.

Dar es Salaam. Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amezungumzia suala la utekwaji na kusema kuwa endapo watajaribu kumteka atapiga picha kwa kutumia simu yake kwanza na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kisha ndipo ataondoka na watekaji hao.

Akizungumza kanisani kwake leo, Gwajima alisema  Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam ndiye anayejua alipokuwa mwanamuziki Roma Mkatoliki.

“Nampenda sana Rais wangu, lakini huyu Bashite analeta picha mbaya. Alisema atapatikana kabla ya Jumapili maana yake unayeee,” alisema