Upelelezi wazidi kukwamisha kesi ya Kitilya na wenzake

Muktasari:

 Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni  kwa  Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Dar es Salaam.Upelelezi wa kesi inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry  Kitilya, mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi  Solomon katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamili.

Wakili wa Serikali, Hellen Moshi aliyaeleza hayo leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Hata hivyo Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashtaka Juni 2, 2017 kueleza upelelezi umefikia katika hatua ipi.

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni  kwa  Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Wanadaiwa kula njama na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, Kwa upande wa mshtakiwa.