DC awakalisha kitako watumishi

. Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Festo Kiswaga.

Muktasari:

  • Hospitali hiyo ambayo inahudumia wilaya tatu za Mkoa wa Simiyu, inalalamikiwa kwa muda mrefu na wananchi kuwa, viongozi wake wameshindwa kushughulikia tatizo la uzagaaji   taka kila kona.

Bariadi. Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Festo Kiswaga ametoa siku saba kwa Katibu wa Afya wa Hospitali ya Somanda kushughulikia tatizo la uchafu wa mazingira maeneo yanayoizunguka hospitali hiyo.

Hospitali hiyo ambayo inahudumia wilaya tatu za Mkoa wa Simiyu, inalalamikiwa kwa muda mrefu na wananchi kuwa, viongozi wake wameshindwa kushughulikia tatizo la uzagaaji   taka kila kona.

Hali hiyo ilimlazimu mkuu wa wilaya hiyo kufanya kikao na watumishi kuwakumbusha wajibu na majukumu yao, wanayopaswa kuyatekeleza.

Kiswaga alimtaka katibu huyo kutenga bajeti maalumu ya usafi ili kuhakikisha vifaa na shughuli zinakwenda bila kukwama.