Kusuasua kwa uchumi kikwazo kwa CRDB

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei

Muktasari:

  • Mkutano mkuu wa 22 wa CRDB unaendelea jijini Arusha leo (Jumamosi)
  • "Ujazo mkubwa wa fedha ulikua kwa asilimia 2.5, mdogo zaidi kwa miaka ya hivi karibuni. Bado serikali ilihamisha Sh700 bilioni kutoka benki za biashara kwenda BoT, haya yote yalikuwa kikwazo cha kustawi kwa uchumi hasa sekta ya fedha,"  amesema Dk Kimei.

Arusha. Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei amesema kutokana na hali ya uchumi kutokuwa nzuri mwaka Jana, benki iliahirisha mpango wake wa kufungua matawi nchini Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

"Ujazo mkubwa wa fedha ulikua kwa asilimia 2.5, mdogo zaidi kwa miaka ya hivi karibuni. Bado serikali ilihamisha Sh700 bilioni kutoka benki za biashara kwenda BoT, haya yote yalikuwa kikwazo cha kustawi kwa uchumi hasa sekta ya fedha,"  amesema Dk Kimei.

CRDB ni benki pekee ya Tanzania yenye matawi nje ya nchi. Tayari inatoa huduma nchini Burundi ambako ilifanikiwa kupata faida ya Sh2.3 bilioni kabla ya kodi mwaka Jana.