Makamba ataka jitihada zifanyike kunusuru mazingira Kasulu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira na Muungano), January Makamba

Muktasari:

Makamba ametoa kauli hiyo, baada ya kupata taarifa ya utekelezaji wa hifadhi wa mazingira na changamoto zake kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi.

Kasulu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira na Muungano), January Makamba amesema  kunahitajika jitihada mahususi za uhifadhi wa mazingira kwenye wilaya ya Kasulu   baada ya kuharibiwa kimazingira.

Makamba ametoa kauli hiyo, baada ya kupata taarifa ya utekelezaji wa hifadhi wa mazingira na changamoto zake kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi.

Kanali Mkisi alimweleza Makamba kuwa Kasulu ni miongoni mwa wilaya zilizoathiriwa na uharibifu wa mazingira kutokana  uchomaji wa misitu, wahamiaji haramu wanaoharibu vyanzo vya maji na wimbi la mifugo.

Makamba amesema Serikali itahakikisha inapambana na hali hiyo katika wilaya hiyo ili Kasulu na Kigoma kuwa katika hali nzuri ya mazingira.