Tuesday, April 18, 2017

TPSF yaitaka serikali kushirikiana na wafanyabiashara

Mkurugenzi  wa chama cha waajiri nchini Aggrey

Mkurugenzi  wa chama cha waajiri nchini Aggrey Mlimuka 

By Colnely Joseph, Mwananchi Cjoseph@mwananchipapers.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta binafsi nchini (TPSF) imeiomba Serikali kushirikiana na wafanyabiashara katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili iweze kusaidia kuongeza mapato na kutoa ajira zaidi.

Akizungumza leo Jumanne katika mkutano wa kujadili na kukagua ripoti ya awali ya biashara,  Mkurugenzi  wa chama cha waajiri nchini Aggrey Mlimuka amesema endapo mazingira ya biashara yataboreshwa itakua ni tija kwa taifa hususani katika vita ya ukosefu wa ajira.

"Kuna umuhimu mkubwa wa kujadili maboresho ya aina hii na lengo ni kuboresha mazingira ya biashara nchini kwani kwa kufanya hivyo Serikali na sekta binafsi zote zitanufaika hususani kimapato" amesema.

 

 

-->