Wananchi hifadhini chakula’

Muktasari:

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Mbaazi Msuya amesema jana kuwa hali hiyo itasababisha ukame na tishio la njaa katika baadhi ya maeneo ambayo hutegemea mvua katika kilimo.

Dar es Salaam.Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuhifadhi chakula baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kutabiri kuwa kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu, maeneo mengi ya nchi yatakuwa na mvua zitakazonyesha chini ya kiwango huku maeneo mengine yakikumbwa na ukame.

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Mbaazi Msuya amesema jana kuwa hali hiyo itasababisha ukame na tishio la njaa katika baadhi ya maeneo ambayo hutegemea mvua katika kilimo.

Msuya amesema kutokana na utabiri wa TMA, wananchi wanashauriwa kulima mazao ya muda mfupi na yanayostahimili ukame. “Maofisa ugani wanatakiwa kutoa ushauri kwa wananchi kuhusu mazao wanayotakiwa kupanda kwenye maeneo yao,” amesema.