Makonda aanza maandalizi ya ‘Mti Wangu’ Oktoba Mosi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Muktasari:

Makonda amesema  miti itakayopandwa Oktoba Mosi, itamwagiliwa na maji ya bomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasco)  badala ya kutegemea  mvua pekee.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amefanya ziara katika barabara ya Airport na Barack Obama ikiwa ni  maandalizi ya kampeni ya ‘Mti Wangu’ inayotarajiwa kuzinduliwa Oktoba Mosi .

Makonda amesema  miti itakayopandwa Oktoba Mosi, itamwagiliwa na maji ya bomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasco)  badala ya kutegemea  mvua pekee.

"Kila mwananchi anatakiwa kuhakikisha anapanda mti na kuusimamia ukue ndipo tutaweza kufikia lengo letu la kupanda miti 4 millioni, wamiliki wa viwanda wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kwani viwanda ndivyo vinaongoza katika uchafuzi wa mazingira,"alisema Makonda.

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema alisema:

 "Baada ya kupanda miti hiyo katika eneo la Airport utafuata mkakati wa kuweka mawasiliano ya intaneti bure katika vituo vya karibu ili mtu anapokuwa maeneo hayo apate huduma ya mtandao" alisema

Kwa taarifa hii zaidi na nyingine nyingi  nunua gazeti lako la Mwananchi kesho au soma mtandaoni BONYEZA HAPA