Lukuvi ataka mapendekezo ya gharama za kupima ardhi yatolewe

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Muktasari:

Akifungua kongamano na mkutano wa mwaka wa wapima ardhi leo (Jumatano), Lukuvi amesema utaratibu wa sasa kutowekwa wazi gharama za kupima viwanja na mashamba unawakatisha tamaa wananchi.

Dar es Salaam.  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza uongozi wa Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) kutoa mapendekezo ya gharama za kupima ili Serikali iweze kuwatangazia wananchi.

Akifungua kongamano na mkutano wa mwaka wa wapima ardhi leo (Jumatano), Lukuvi amesema utaratibu wa sasa kutowekwa wazi gharama za kupima viwanja na mashamba unawakatisha tamaa wananchi.

Lukuvi amesema wengi hawapimi ardhi na kusababisha Serikali ikose mapato ya kodi.

Amesema gharama za kupima zikiwa nafuu na kuwekwa wazi wananchi wengi watapima viwanja na kupewa hati.

Awali Rais wa IST, Martins Chodota aliiomba  Serikali kuweka uzio ardhi inayotumika kwa ajili ya mifugo ili kuondoa migogoro.