Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hoja sita za rufaa ya Lema kusikilizwa leo

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema .

Muktasari:

Wakili Sheck Mfinanga anayemwakilisha Lema alisema waliwasilisha hoja hizo za rufaa kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana mteja wao.

Arusha. Hoja sita za mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kupinga kunyimwa dhamana zinatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Salma Maghimbi.

 Wakili Sheck Mfinanga anayemwakilisha Lema alisema waliwasilisha hoja hizo za rufaa kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana mteja wao.

 Lema aliyekamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma, tangu wakati huo anashikiliwa kwenye Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha ambako amekaa kwa siku 56.

 Baada ya kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Lema alipewa dhamana na Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 akidaiwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

 Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama kumpa dhamana mbunge huyo.

Mawakali wa Lema nao walikata rufaa kupinga mteja wao kunyimwa dhamana ambayo imepangwa kusikilizwa leo baada ya kukwama kwa muda mrefu kutokana na kuwapo pingamizi za kisheria zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

 Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi